Madereva wagoma kutoa ushuru wa kutoka geti la stendi kuu ya Njombe



MADEREVA wa madasi yaendayo wilaya na mikoa jiranni ya Njombe wamegoma kulipa ushuru wa geti la kutoka stendi hiyo kutokana na tope lililopo katika eneo hilo la stendi na kuwapa shida abiria wao na kuiomba halmashauri kufanya ukarabadi wa eneo la stendi kwa kujaza kifusi ili waendelee kulipa ushuru.

Awali asubuhi jana madereva hao walipaki magari yao nje ya stendi ikiwa ni njia ya kuishinikiza serikali kuondoa tope lililojaa katika stendi hiyo na baadae kukubaliana kuingia stendi lakini kwa makubaliano ya kuto lipa uhuru get nla kutokea.

Wakizungumza kwa jazba madereva, abiria na maafisa usafilishaji wamesema kuwa haiwezekani halmashauuri hiyo kuendelea kuchukua ushuru huku katika stendi hiyo hakuna marekebisho wanayo yafanya wakati wanachukua ushuru.

Kelvini Nyepe ni moja ya viongozi wa wakatisha tiketi katika stendi hiyo alisema kuwa waliamua kubadisha ambiria wao nje ya steni kutokana na stendi hiyo kuwa na tope kama shamba la mpunga na kuwaonea huruma wateja wao wanao safiri kuchafuka na tope hilo.

“Tulitoa mabasi yote nje ya Steni ili kuonyesha kuwa hatukubali abiria wetu kuchafuka katika stendi hii lakini tumeona gari zikiwa nje ya stendi hakuna usalama kwa kuwa kunaweza kusababishwa ajari kwa watu wasio husikahivyo tumeamua kuingia stendi kwa sharti la kuto lipa ushuru hadi stendi itakapo rekebishwa,” alisema Nyepe.

Mwenyekiti wa wasafiri shaji Laiton Mwaipopo aliesema kuwa kuwa eneo hilo ni chafu na linahitaji marekebisho na kuwa wamefika katika ofisi za halmashauri na kuahidiwa kuwa watarekebishiwa katika eneo hilo la stendi.

“tumeamua kuingiza gari ndani ya stendi kwaajili ya usalama na tumekubaliana kuto lipa ushuru gali zote zitakazo  ingia ndani ya stendi hiyo,” alisema Mwaipopo.

Dereva wa Texi zinazo paki katika stendi hiyo alisema kuwa wamekuwa wakikosa wateja tangu kuanza kwa tope hilo lililodumu kwa muda wa wiki mili sasa na kuwa halmashauri haifanyi kufanya ukarabati kwa kuwa tepe wanaliona lakini hawafanyii kazi na kuwa kila walipo wafuata wanaambiwa kuwa stendi hiyo sio stendi na ipo eneo la Tanraod na wamewekeza nguvu kwenye stendi mpya inayo jengwa.
Aidha mmoja wa abilia amesema kuwa eneo hilo limekuwa ni chafu hadi kufikia hatua ya kubebwa mgongoni kutokan ana tope lililojaa huku abiria wengine wakisubiri kupanda magari nje ya stendi ili kuto chafuka na tope.

Kwa upande wa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Mjini Edwin Mwanzinga alisema kuwa ukarabati katika stendi hiyo utafanyika baada ya kumalizika kwa mvua zinazoendelea kunyesha na kusema kuwa katika stendi hiyo gari zinatembea ni afadhari kuliko barabara za vijijini hizo ndio zimejifunga kabisa.


Hata hivyo mkurungenzi wa halmashauri ya mji wa njkombe hakuweza kupokea siku ili kuzungumzia tatizo la stendi hiyo.