Facebook inasherehekea miaka
kumi wiki hii tangu kuzinduliwa. Ina watumiaji bilioni 1.2. Lakini nani
anatumia Facebook and wanaitumia kwa njia gani?
Mishumaa kwenye keki ya Facebook
inaposherehekea miaka 10 haitazima kabla ya mtu kuwa na tashwishi ikiwa
kampuni hiyo itadumu na kufikisha mwaka wake wa 11.Katika utafiti uliofanywa hivi karibuni, ikiwa utaaminika , siku za mwisho za Facebook zinakaribia.
Taarifa mbali mbali zinapendekeza kuwa idadi kubwa ya watumiaji wa Facebook , vijana wakiwemo wengi, wanachoshwa na mtandao huo wa kijamii baadhi ya watafiti wakisema kuwa watumiaji wengi wanalinganisha Facebook na maradhi mabaya.
Utafiti kama huu ambao huambatanishwa na picha ya Mark Zuckerberg mwasisi wa mtandao huo akionekana mwenye huzuni huonyeshwa sana na vyombo vya habari na hata kusambazwa zaidi kwenye Facebook.
Kwa hivyo wakati watafiti waliposema kuwa kampuni hiyo itapoteza asilimia themanini ya watumiaji wake katika kipindi cha miaka mitatu, wakuu wake walijibu kwa ukali.
Facebook ina watumiaji wengi zaidi vijana kuliko mtandao mwingine wowote.
Imekuwa ikibadili sura yake tangu mwaka 2004.
Vijana wengi wanasema waliacha kutumia Facebook kwa sababu ya wazazi wao, ambao pia wamejiunga na mtandao huo wa kijamii.
Wazazi hutuma picha za watoto wao kwenye mtandao ambazo wao wenyewe wanahisi ni za kuchekesha.Jambo hili limewatia aibu vijana ambao wameamua kutumia mitandao kama WhatsApp au Snapchat badala ya kuwa kwenye mtandao mmoja na wazazi wao.
Licha ya vijana wanaotumia Facebook kupungua watu wenye umri zaidi ya 55 wameonekana kuongezeka.