ZIARA YA KIKAZI YA RAIS MAGUFULI YAKAMILIKA NDANI YA SIKU 7 KATIKA MIKOA MINNE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Julai, 2017 amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kwa kufungua barabara ya Itigi – Manyoni Mkoani Singida.
Barabara hiyo inayounganisha Mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma ina urefu wa kilometa 89.3 na imejengwa gharama ya Shilingi Bilioni 114.692, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza na wananchi wa Itigi katika sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, amesema Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa barabara hiyo pamoja na nyingine saba alizozifungua katika ziara hii zenye urefu wa jumla ya kilometa 707 zimejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 806, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba Serikali imeamua kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini kwa lengo la kuhakikisha barabara za vijijini zinajengwa kwa kiwango cha lami.
Kwa barabara ya Mkiwa – Itigi yenye urefu wa kilometa 57 na ambayo tayari zabuni ya ujenzi ilishatolewa kwa mkandarasi ili aijenge kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 104, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuupitia upya mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa kiwango cha fedha kilichopangwa ni kikubwa ikilinganishwa na gharama halisi.
Pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa kujadiliana na Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili aweze kuendelea kujenga barabara kutoka Itigi kuelekea Chunya hadi Makongorosi Mkoani Mbeya.
Pamoja na wananchi wa Itigi Mkoani Singida, Mhe. Dkt. Magufuli aliyetokea Tabora amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Kigwa, Kizengi na Tura Wilayani Uyui na amewataka kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa pamoja na kuzingatia uzalishaji mazao yanayostahimili ukame kama vile uwele, mtama, viazi na muhogo ili kuepuka tatizo la upungufu wa chakula.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kuhamasisha wananchi kufanya kazi hususani shughuli za kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa Taifa, na ameonya kuwa kiongozi ambaye hatatekelezi agizo hilo atakuwa hafai na ataondolewa.
“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hamasisheni watu kufanya kazi na kama kuna viongozi na watendaji wasiotekeleza wajibu huo katika maeneo yenu waondoeni mara moja” ameagiza Mhe. Rais Magufuli.
Viongozi wengine waliongozana na Mhe. Rais Magufuli katika ziara ya leo ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King na Wabunge wa Mkoa wa Singida.
Mhe. Rais Magufuli amewasili katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wananchi Kijiji Cha Tula Uyui Mkoani Tabora waliojitokeza Barabarani Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo akiawa njiani katika moja ya mikutano ya barabarani kwa waliojitokeza Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati Rais alipowasili Mkoani Singida eneo la Itigi ili kufungua Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa na Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Itigi na Manyoni wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017.Wananchi wa Itigi na Manyoni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatubia kwenye Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wapili kushoto na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida,wakiondoa kitambaa kuashiria Kufunguliwa Rasmi kwa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida na Tabora Wakikata Utepe kama ishara ya kufunguliwa Rasmi kwa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiteta jambo na Wang Chao mwakilishi wa Pawer China Internatinal Group Limited wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwasalimia kwa kupunga mikono kwa wananchi wa Itigi na Manyoni walioshiriki na Kushuhudia Ufunguzi wa Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja,Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye Ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kwa Kupitia Singida hadi Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma Julai 25,2017

from Blogger http://ift.tt/2v7gUF7
via IFTTT