PROF. MJEAMA 'WAHITIMU BIASHARA WASIKATE TAMBAA'

PROFESA EMMANUEL MJEMA AWAFUNDA WAHITIMU WA CBE KAMPASI YA MBEYA.


Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Profesa Emmanuel Mjema,akizungumza na Wahitimu wa mafunzo ya ujasiliamali alipokuwa mgeni wakati wa kufunga semina ya Ujasiliamali kwa Wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya


Mwenyekiti wa Umoja wa Wahitimu waliosoma CBE Kanda ya Nyanda za juu kusini (ALUMNI) Boyd Mwakyusa, akitoa neno la utangulizi katika hafla ya kufunga mafunzo ya ujasiliamali kwa wahitimu wa CBE Kampasiya Mbeya

Katibu wa Alumni, Graciano Kunzugala, akiwashukuru washiriki wa Mafunzo ya Ujasiliamali waliyoyapata wahitimu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya

Profesa Mjema akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya ujasiliamali kwa wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya.

Baadhi ya washiriki wa semina ya ujasiliamali wakisubiri kutunukiwa vyeti vya ushiriki wa mafunzo waliyopata

Mkurugenzi wa CBE Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akimwelekeza jambo Mwenyekiti na Katibu wa ALUMNI Kanda ya Mbeya

Profesa Mjema akimtunuku Cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiliamali mmoja wa Wahitimu wa Chuo cha CBE Kampasi ya Mbeya.

Mhitimu wa CBE akipongezwa na Mkurugenzi wa Kampasi ya Dodoma

Mkurugenzi wa Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akimpongeza mmoja wa wahitimu wa CBE Mbeya baada ya kutunukiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiliamali

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi na baadhi ya Watumishi wa CBE baada ya kufungwa kwa mafunzo ya ujasiliamali

Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya ujasiliamali wakionesha vyeti vyao katika picha ya pamoja na viongozi wa CBE na waandaaji wa mafunzo


MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema,ametoa wito kwa wahitimu wa vyuo kutokata tama katika utafutaji wa maisha.

Profesa Mjema ametoa wito huo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili ya Ujasiliamali kwa Wahitimu wa CBE Kampasi ya Mbeya yaliyomalizika katika ukumbi wa Hoteli ya Livingstone.

Profesa Mjema ambaye pia aliwatunuku vyeti vya kuhudhuria mafunzo hayo wahitimu alisema katika utafutaji wanapaswa kuwa na uvumilivu hivyo hawatakiwi kukata tama mapema.

Aidha aliwataka wahitimu hao kuitumia kwa vitendo elimu ya ujasiliamali walioipata kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika jamii.

Mkuu huyo wa Chuo pia aliwapongeza waandaaji wa mafunzo hayo ambao ni umoja wa wahitimu waliosoma zamani CBE(ALUMNI) kanda ya Nyanda za juu kusini.

Alisema kitendo walichokifanya ni uzalendo wa kukipenda Chuo kwa kurudisha fadhila ambayo wameitoa kwa wahitimu.

Alisema jukumu la wahitimu ni kukishauri Chuo juu ya mabadiliko mbali mbali na kukijulisha juu ya mambo yanayokuwa yakiendelea nje ya Chuo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa ALUMNI Kanda ya Nyanda za juu kusini, Boyd Mwakyusa alisema mafunzo hayo yamehudhuriwa na washiriki 88.

Alisema lengo la mafunzo ni kuwafanya wahitimu kutohangaika pindi wanaporudi uraiani badala yake wajue fursa za kuzitumia ikiwa ni pamoja na kujishughulisha na ujasiliamali.

by Mbeya Yetu Blog