Tahadhari..Kuwa Makini na Kofia za Helment za Bodaboda..Wanazipaka Dawa Zitakazokupoteza Fahamu Ili Wakuibie..Sambaza Ujumbe Huu kwa Mwezako..!!!

Hii imenitokea tarehe 28/05/2017 maeneo ya ubungo 
Iko hivi hawa jamaa waendesha bodaboda wamebuni mbinu mpya za kuwaibia wateja wao.
Niipanda Boda Boda pale ubungo river side baada ya kumweleza naelekea wapi nikapewa kofia (helmet) nikavaa ,baada ya kuivaa mara moja dereva alianza safari na akawa anaendesha mbio ilikuwa jioni ya saa 1:30 kwenda saa mbili usiku.
Kitendo cha kusogea mbele kidogo nilianza kuishiwa nguvu huku Dereva naye akianza kupotelea machochoroni baada ya muda mfupi nilipoteza fahamu sikuwa najitambua tena .
Ilinichukua masaa kama matatu hivi kuja kuzinduka kutoka usingizini,wakati huo nilijikuta vitu vyangu vyote nilivyobeba sikuwa navyo ikiwa ni pamoja na pesa kiasi cha shs 180,000 pamoja na laptop yangu na vitu vingine .
Hivyo nawaonya mnaopanda bodaboda muwe makini hasa nyakati za usiku helmet Inapakwa madawa yanayosababisha kuishiwa nguvu kabisa na hii haijalishi mwanamke ,mwanaume kuweni makini na madereva msiowajua.

from Blogger http://ift.tt/2rVDKhe
via IFTTT