UNSC: Kikosi cha kulinda amani kutumwa Mali


UNSC: Kikosi cha kulinda amani kutumwa Mali
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza juu ya kutumwa haraka kikosi  kingine  cha kulinda amani cha umoja huo nchini Mali. 
Taarifa iliyotolewa jana mjini New York imeeleza kuwa, Baraza la Usalama limelazimika kuchukua hatua hiyo ya dharura baada ya Ufaransa kutangaza azma ya kupunguza wanajeshi wake walioko nchini humo.
Umoja wa Mataifa unachukua maamuzi ya kutuma wanajeshi zaidi wa kulinda amani nchini Mali katika hali ambayo hivi sasa umoja huo una askari wake 5,500 tu,  jumla ya wanajeshi 11,200 wa kulinda amani walioko nchini humo. 
Ufaransa ambayo ina wanajeshi zaidi ya 2,500 nchini Mali inakusudia kupunguza wanajeshi wake hadi kufikia 1,000 ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Wakati huohuo Bert Koenders Kamanda wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA amesema kuwa, kuna udharura wa kutumwa askari zaidi wa kulinda amani  kutokana na kuendelea mapigano nchini humo.
Na Kiswahili.irib.ir