Maduka siku tatu yafungwa Njombe

WANANCHI Mkoani Njombe na mji wa makambako wa siku tatu wamekodsa huiduma muhimu katika maduka yao ambapo madukwa yakiwa yametiwa makufuri kwa siku tatu mfululizo kwa kile walichodai wafanyabiashara kuachiwa kwa mwenyekiti wao Jonson Minja ambaye dhamana yake ilifungwa.

Adha ya kukosekana kwa bidhaa muhimu katika miji hiyo mkoani Njombe imeanza siku ya Alhamisi na kuendelea hadi siku ya Jumamosi ambapo wafanyabiashara walikaa kikao cha ndani na kujadili mambo yanayo wahusu huku wakizuia waandishi wa habari kuhudhulia.

Kufungwa kwa maduka kumekuja kufuadia kuwapo kwa kesi ya mfanyabiashara na mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara taifa (JWT) Jonson Minja ambapo siku ya kwanza ya kufungwa kwa maduka ndio kesi yake ili kuwa ikisikilizwa.

Hii ni awamu ya tano tangu kuzwa kwa kufungwa kwa maduka katika mkoa wa Njombe kwa kisingizio cha kwenda kusikiliza kesi ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakifunga maduka pindi wanapo enda kusikiziza kesi za wafanyabiashara wenzao ambao wanashitakiwa na mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) ambapo mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi alitoa tamko la kulaani kufunga maduka.

Dkt. Nchimbi akizungumza katika moja ya mikutano mkoani humo alisema kuwa wafanyabiashara wanacho kifanya siop sahihi kufunga maduka na kuwa wanawakosea sana wananchi wanao wategemea kwa huduma mbalilmbali.

Aliapa kupambana na mtu anaye washawishi wenzake kufunga maduka na kula sahani moja nae na kumfikisha katika vyombo vya sheria ili kumshitaki kwa kile wanacho kifanya.

“Wafanyabiuashara mnacho kifanya sio sahihi naapa kula sahani moja na yeyote atakaye bainika kusambaza na kushawishi wafanyabiashara kufunga maduka…… maduka haya ni ya mama waja wazito wagonjwa ambao hospitalini wameambiua wakanunue vitu madukani wanakuta maduka yamnefungwa,” alisikika kasema kwa uchungu Dkt. Nchimbi baada ya kufungwa kwa maduka mara ya pili.

Kauli hiyo imeendelea kupuuzwa na wafanyabiashara na kuendelea kufunga maduka na mmoja wa fanyabiashara akisema kuwa kufungua na kufungwa kwa maduka kupo mikonono mwao.

Mfanyabiashara huyo ambaye kakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa wanapo enda kusikiliza kesi wanahoifia kukosema mahesabi ndio maana wanafunga maduka ili wakae mahakamani kwa uhuru bila ya mawazo ya biashara.

Aidha Elimtaa ilikutana na mfanyabiashara ambaye duka lake la vitu ya Stationali ililikuta likiwa wazi na kuliambia kuwa hawezi kufunga duka wakati kesi ikombali na eneo alilopo yeye na huko ni kujiingiza hasara.

Edwini Mwanzinga mfanyabiashara na mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Njombe alisema  kuwa haoni mantiki ya kufunga maduka ili hali kesi iko mbali na kwamba wanaofunga maduka hawajajua wanacho kifanya kwa kuwa hata wasipofungua maduka yao bado watalazimika kulipia kodi yao katika mamlaka husika.

“Nawashangaa wafanyabiashara Dodoma kwenye kesi hawajaenda lakini wanafunga maduka yao na kali zaidi wanafunga halafui wanakaa karibu na maduka yao ndio ujue kuwa hapendi kushinda nyumbani,” alisema Mwanzinga.

Kwa upande wake Mwneyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Makambako, Sifael Sigalla ambaye alizungumza kwa simu kutoka Dodoma alisema wanalazimika kufunga maduka ili kufuatilia mwenendo wa kesi ya Minja na kwamba Mahakama imemnyima dhamana na kesi kuahirishwa bila kutajwa ni lini itaendelea.

Kufuatia mgomo huo ambao unaendeshwa na wafanyabiashara wote nchini badhi ya wadau na wanasiasa waliweza kutoa maoni mbalimbali ambapo baadhi yao walisema kuwa ni vyema wafanyabiashara wakaongeza muda wa mgomo ili serikali iweze kutafuta suluhu kwa sababu inatakiwa ifike wakati haki ikatendeka ili wafanyabiashara waweze kutimiza malengo.

Mmoja wa wadau hao ambaye ni kutoka taasisi ya isoyo ya seruikali Alatanga Nyagawa alisema kuwa wafanyabiashara ilifaa hata vituop vyta mafata vingefungwa hoteli na kuionyesha serikali kuw awanacho fanyiwa sio haki na kuwa wafanyabiashara hao wanahitajika kulejesha marejesho katika mabenko mbalimbali ambayo wamekopa lakini wanakutana na vikwaza mbalimbali ambavyo vina bana haki zao.