NAIBU Waziri wa Fedha, Mwiguru
Mchemba, amemtaka mkuu wa wilaya ya Njombe kutekeleza ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) wanapofanya shughuli mbalimbali katika maeneo ya mji ikiwemo ondoa
ondoa machinga maeneo ya mji.
Mchemba ameyasema hayo wakati akizungumza
na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Njombe wa CCM ambao uliambatana na
uchaguzi, alisema kuwa machinga wasiondolewa katika maeneo ya mji.
Alisema kuwa machingwa
wanapoondolewa katika maeneo ya mji waandaliwe maeneo ya kwenda bila kuwaandalia
maeneo ya kwenda uondoaji huo utakuwa ni kinyume cha ilani ya CCM.
“Kila kinacho fanyika katika mji na
mamlaka za miji au halmashauri ni utekelezaji wa ilani mkuu wa wilaya unatakiwa
kupima kama kina endana na ilani ya CCM ama hakiendani kama kinalenda kwenda
kinyume na ilani basi mkuu wa wilaya ukisimamishe kwani wanao fanya kinyume na
ilani wanahujumu chama,” alisema Mchema.
Wanao wafukuza wakinamama wanao uza
vitu mitaani, vijana walio katika shughuli za kibiashara halali bila msini na
kuwasumbua kwa ushuru wakati wanaacha kukusanya mapato katika vyanzo vikubwa
wana fanya hujuma.
“Wakinamama hawa wakisumbuliwa
wakati wanafanya shughuli zao watasema serikali hii sio ya kuichagua na
wataalamu wa mahesabu wanasema kuw akitendo hicho kita punguza kura nyingi, na
hawa vijana wanaofukuzwa wanaweza kwenda kufanya shughuli zisizofaa,” aliongeza
Mchema.
Kwa upande wao machinga mkoani
Njombe wamelalamikia mikakati inayo fanywa na wilaya hiyo kutokana watendaji wa
mitaa kuzunguka katika maeneo yao kuwanyanayasa kwa kuwafukuza maeneo wanayo fanyia
biashara bila kuwaonyesha sehemu yakufanyia biashara ambayo itakuwa ni rafiki
kwa biashara zao.
Shadrack Pilani alisema kuwa
wamekuwa wakifukuzwa katika mji wa Njombe kufanya biashara kitu kinacho
sabababisha biashara yao kuwa ngumu na kushindwa kumudu maishayao ya kila siku
na kuwa wamekuwa wakipeleka watoto wao shule na kuendesha shughuli za kilipo
kutokana na shughuli hizo.
Alisema kuwa serikali inapo
wafukuza katika maeneo hayo waangale mahali wanapo wapeleka kwani katika mji wa
Njombe awali kuna sehemu walionyeshwa wakafanye biashara zao lakini katika
sehemu hizo si lafiku kwa kufanya biashara zao.
Alisema kuwa walipelekwa katika
machingio ya ng’ombe ambako walitakiwa kufanyia biashara yao huko walishindwa
kufanya biashara kutokana na maeneo hayo sio mapito ya watu kwania biashara yao
inategemea maeneo ambayo kuna mapito ya watu.
Fukuza fukuza machinga maarufu kama
safisha mji mkoani Njombe imeanza mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu huku
machinga wakilalamikia kuto onyeshwa eneo la kwenda kufanyia biashara zao na
kuwa hawajawahi kukaa na uongozi kujadili juu ya mstakabali wa timuatimia na
wapi wanede ambapo na wao wakatoa mawazo yao mahara pakwenda kufanyia biashara.