NAIBU katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa mashambani (Tpawu),
John Vahaye amesema kuwa tukio walilofayiwa wafanyakazi wa kiwanda cha Kibena
tea mwezi uliopita ulisababishwa na uongozi wa kiwanda kupeleka ujumbe tofauti
polisi ambao uliwafanya polisi kufanya walichokofanya siku ya tukio.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe, alisema
kuwa tukio lililofanywa na polisi mwishoni mwa mwezi uliopita la kupiga
wafanyakazi kiwandani hapo lilitokana na taarifa walizo zipata kutoka kwa
uongozi wa kiwanda hicho kuwa kutakuwa na vurugu.
Vahaye alisema kuwa alipata taarifa kupitia kwa viongozi
wake kuhusiana na tukio hilo na amaamua kuja mkoani Njombe ili kupata ukweli wa
tukio hili na kuwa amezungumza na jeshi la pilisi na kuambiwa kuwa
kilichofanywa na jeshi hili kilitokana na taarifa zilizo patikana na kutoka
kiwandani ya kuwa huenda kungekuwa na machafuko na kuwa waliamua kwenda wakiwa
wamejiandaa.
Alisema kuwa amezungumza pia na uongozi wa kiwanda hicho na kukili
wawaita polisi na kuwa waliwapa taarifa na kuwa walihisi kama kungekuwa na
vurugu kubwa lakini polisi walipo fika katika kiwanda hicho walikuta
wafanyakazi majira ya saa 10:00 usiku wakikusanyana hivyo walihisi kutakuwa na
vurugu.
“Nimekutana na pande tatu jeshi la polisi, uongozi wa
kiwanda, na tawi la Tpawu kiwandani na kupata maelezo ya pande zote na kubaini
kuwa uongozi wa kiwanda ndio uliofanya makosa kutokana na taarifa walizo zitoa
polisi na polisi walivyo zipokea,” alisema Vahaye.
Alisem akuwa uongozi wa Tpawu kiwandani hapo ulisema kuwa
wafanyakazi hao walikuja kuwandani hapo wakiwa wanajiandaa kwa mkutano wa saa
2:00 asubuhi ambao walikubaliana kufanyika januari 26 katika mkutano wao wa
januari 3 mwaka huu ambapo uongozi ulibadilisha mawazo hayo na kutaka mkutano
huo ufanyike siku hiyo majira ya saa 9:00 alasiri.
Alisema polisi bila kuuliza walifanya kile kilicho tokea cha
kupiga wafanyakazi bila kujua nini kilkicho wapeleka kutoikana na taarifa
walizi zipata kutoka kwa uongozi.
Vahaye alisem akuwa kwa kile kilicho fanywa na jeshi la
polisi hakiwezi kutatua migogoro ya wafanyakazi mahara pa kazi baina yao na uongozi
wa sehemu hiyo na kuwa sheria haisemi polisi wahusishwe katika utatuzi wa
migogoro.
Hivyo alisema kuwa katika mkutano wa wafanyakazi hao Februari
23 ofisi ya katibu mkuu wa chama hicho itahudhuria mkutano huo na kufuatilia
kwa karibu juu ya kilekitakacho fanyika katika mkutano huo.
Alisema kuwa wafanyakazi hao madai yao ambayo yalisababisha
mkutano huo ambao haukufanyika januari 26 ni yakweli na madai hayo yameanza
kudaiwa kwa muda wa miaka 6 sasa tangu iwasilishwe kwa uongozi wa kiwanda
hicho.
Vahaye alichukua fursa hiyo kuwataka wafanyakazi katika
mahara pakazi na uongozi kuhakikisha wanafuata sheria na sio kutumia vyombo vya
dola katika utatuzi wa matatizo.
Aidha katika tukio hilo ambalo wafanyakazi wa kiwanda cha
hai walivamiwa katika kambi zao na kupewa kipigo na askali ambao walikuwa 32
kwa mujibu wa Vahaye watu 9 walipelekwa hospitalini kupatiwa matibabu kutokana
na kipigo walicho kipata.