MADIWANI
wa halmashauri ya wilaya ya Njombe wamemuagiza mkurugenzi wa halmashauri
hiyo kusimamia kikamilifu idara ya elimu wilayani humo kufuatia kushuka kwa
ufaulu wa wanafunzi wa shule za misingi mwaka jana na kupelekea shule za
wilaya hiyo kutoingia katika shule kumi bora za mkoa.
Wakizungumza katika kikao
cha baraza madiwani, wamesema ufaulu umeshuka kwa kiasi
kikubwa kutokana na afisa elimu msingi na mkurugenzi kushindwa
kuwasimamia waratibu elimu na walimu kwa kuwa walimu hao hawakai kwenye
vituo vyao vya kazi wakijishughuluisha na kilimo pamoja na kupanda miti
ya mbao.
Akichangia hoja ya waalimu
kufanya shughuli zingine mbali na waliyo ajiuliwa na serikali Diwani wa kata ya
Ninga, Paulo Kinyamagoha, alisema kuwa waalimu hao wamekuwa wenyeji mpaka
wanaanza kufanya shuguli ambazo ni tofauti ambazo wameajiliwa.
“Waalimu hawa wasipo
simamiwa vizuri wanaanza kufanya shughuli za kilimo na kuacha kufundisha kwani
wengine wamekuwa wenyeji mpaka wanaanza kujishughulisha na kilimo cha miti ya
mbao wengine wanashinda virabuni kwenyepombe za kienyeji, kwa kuwa wamekua kama
wanakijiji,” alisema Kinyamagoha.
Kinyamagoha alitoa ushauri
wa serikali kuwa,” Ushauri wangu kwa serikali ni kuwa hamisha waalimu hawa
wakikaa baada ya muda ili elimu kuwa bora kabra hajaaza kuwa mwanakijiji
ahamishwe,” alisema Kinyamagoha.
Pia katika kikao hicho kumeibuka malalamiko kwa mkurugenzi kuwa ameshindwa kusimamia utoro wanafunzi ambapo zaidi ya wanafunzi 100 katika shule ya msingi Lole kata ya Ikuna wametoroka shuleni na kusababisha migongano baina uongozi wa kata na shule hiyo.
Aidha madiwani hao
wamepongeza hatua ya afisa mtendaji wa kata ya Ikuna ambaye aliamua kuchukua
hatua ya kumkataa mwalimu mkuu wa shule ya Lole kwa kuto simamia mahudhulio ya
wanafunzi kwa kumkaataa katika kikao cha maendeleo cha kata (Kamaka).
Mtendaji huyo alimkaataa mkuu wa shule ya
msingi Lole kwa katika kikao hicho licha ya baadhi ya madiwani kumpongeza
baadhi yao walisema kuwa mtendaji kabla ya kumkataa mtendaji huyo alitakiwa
kumfuata afisa elimu na kumueleza kile kilicho tokea katika shule hiyo kabla ya
kumkataa.
Akijibu tuhuma kwa niaba ya mkurugenzi afisa elimu msingi wilaya ya Njombe Hamisi Milowe pamoja na kukiri kuwa ufaulu umeshuka alibainisha changamoto zinazo pelekea ufaulu kushuka kuwa ni upungufu mkubwa wa walimu pamoja na utoro uliolkithiri kwa wanafunzi.
Milowe alisema kuwa serikali inabanwa na bajeti katika kufanya babadiliko ya waalimu mara kwa mara kama alivyo shauri mmoja wa madiwani na kuwa kunarazimika mwalimu mmoja kukaa sehemu moja kwa muda mrefu.
Mwisho