Wafanyabiashara wafunga maduka njombe kwa siku nzima ya Februari 11







WAFANYABIASHARA wote mkoa wa Njombe Leo Februari 11 waliyafunga kwa siku nzima
maduka yao wakiungana na wenzao kote nchini kupinga kitendo cha mmwenyekiti wa wafanyabiashara taifa, Jonson Minja ambaye Leo alipandishwa kizimbani mjini Dodoma na Kesi yake kuahirishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe, makamu mwenyekiti, korido ya wafanyabiashara mkoa wa hapa (Tccia) Menadi Mlyuka, alisema kuwa wameamua kufunga maduka yao wakumuunga mkono mfanyabiashara mwenzao Minja, pamoja na  kuishinikiza serikali kumuachia ambaye
anakesi mahakamani jijini Dodoma.

Alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuionyesha serikali na umma wa watanzania, kuwa hawajafuarahishwa na kitendo cha kuto kuwa na msimamo kuhusia na mashine za kieletroniki (EFD) na kusababisha wafanyabishara
baadhi yao kupewa mashine na wengine kutoingia katika mfumo wa kutumia mashine hizo.

Mlyuka alisema kuwa wafanyabiashara wameamua kuungana ili kuonyesha msimamao wao na mgomo huo ni mwanzo na wanatarajia kufanya mgomo mwingine wakati wowote na kuonsha serikali kuwa wanaweza kufanya kitu.

Alisema kuwa wanataka nao katika biashara zao wafanye maedndeleo kutokana na kiele wanacho kipata na sio serikali inabyo wafanyia kwa kuwa kwa kufanya hivyo wananyanyasika na kuishia kufanya biashara bila
kufanya maewndeleo.

Alisema kuwa serikali kama itaendelea na mfumo inao utumia kwa kuwanyanyasa wafanyabishara kwa maafisa wa mamlaka ya mapato TRA kuwavamia wafanyabiashara na kuwadai taarifa za biashara wanaweza
kuzuia mapato ya serikali.

"Serikali kama itaendelea hivyo kwa maafisa wake wa tra kuja katika biashara zetu na kutu vamia tunaweza tuka zuia kutoa mapato na tuone kama mambo yataenda," alisema Mlyuka.

Aidha mji mzoma wa Njombe maduka ya jumla na rejareja yalikuwa yamefungwa na kusababisha huduma kuwa ngumu kwa wakazi wa mkoa huo huku wakipata shita watu mbalimbali walio kuwa wakitoka nje ya mji
kununua vitu vya jumla.