WAFANYABIASHARA mkoani Njombe wanatarajia kufunga maduka yao
Machi 3 mwaka huu kwa lengo la kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya
mfanyabiashara mwenzao ambaye amepandishwa kizimbani na mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA) mwezi huu.
Wakizungungumza na waandishi wa hanari mkoani Njombe, wafanyabiashara
hao walisema kuwa watafunga maduka yao na kwenda katika mahakama ya hakimu
mkazi wilaya ya Njombe kusikiliza kesi ya Mexon Sanga, ambaye alipandishwa
mahakamani Februari 6 mwaka huu.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Njombe, Oraph alisema,
Sanga ambaye atasindikizwa na wafanyabiashara mkoani Njombe siku ya kesi yake
ambayo itatajwa Machei 3 mwaka huu na alipandishwa katika mahakama hiyo Ijumaa
mwishoni mwa wiki iliyo pita wafanyabiashara wote watakuwepo mahakamani.
Alisema kuwa baada ya kutoka mahakamani wanatarajia kukutana
na mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi, ili kuzungumza juu ya vitendo ambavyo
wanafanyiwa na mamlaka hiyo kwa kulenga baadhi ya wafanyabiashara kila wanapo
fanya shughuli zao.
“Baada ya kwenda kusikiliza kesi ya mfanyabiashara mwenzetu
tunatarajia kukutana na mkuu wa mkoa katika kikao ya pamoja baina yetu na yeye,
sisi kama wafanyabiashara hatuja furahishwa na mamlaka ya mapato kutoka mkoani
Mbeya na mikoa mingine kuja mkoani kwetu kukusanya mapato na kufanya ukaguzi,
maafisa wa TRA, weamekuwa wakifuata baadhi ya wanyabiashara na kuchukua mapato
kisirisiri,” nalisema Oraph.
Alisema kuwa baadhi ya maofisa wa TRA wamegeuza Njombe kama
shamba la bibi na kuja kuchukua rushwa kwa wafanyabiashara wake kwa kisingizio
ni waoga wakisikia mamlaka hiyo hivyo wameamka na hawata kubaliana.
Alisema wafanyabiashara wengi wamekuwa wakichukuliwa pesa
zao na maofisa hao kisirisiri na pesa hizo kuandikiwa risiti yenye kiwango
tofati na kile wanacho kitoa.
“Tumechoka kuchukuliwa pesa bila mpangilio na kulengwa
baadhi ya wafanyabiashara, pia kitendo cha mwenzetu kupandishwa mahakamani
tutahakikisha haki inapatikana na tutahudhulia mahakamani kila anapo hitajika
kama ishara ya kumuunga mkono,” aliongeza Oraph.
Nao baadhi ya wafanyabiashara manaunga mkono wazo la
mwenyekiti wao na kufunga maduka siku hiyo ya kesi na wote kwenda mahakamani, Maxon
alipandishwa mahakamani Februari 6 mwaka huu kwa mashitaka ya kuzuia mamlaka ya
mapato TRA kufanyakazi katika ofisi yake.
Naye makamu mwenyekiti wa Korido ya biashara mkoa wa Njombe Menad
Mlyuka, alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikiwanyanyasa wafanyabiashara, kwa
kuwaambia wawaonyeshe maghara ya bidhaa zao na vitabu ya mauzo, kasha wanatozwa
hongo.
“Licha ya kuwanyanyasa wafanyabiashra wetu wamekuwa
wakichukua hongo kubwa, kitu hicho kimekuwa kikisababisha wafanyabiashara wengi
kuishia njiani katika safari zao za maendeleo,” alisema Mlyuka.