VIONGOZI wa msakosi hapa nchini wametakiwa kutazama kwa
umakini michanganuo ya wanachama wao wanao hitaji mikopo ili kukabiliana na
tatizo la kuwapo kwa watu wanao shindwa kulipa malejesho ya mikopo yao.
Hayo yamebainishw ana mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani
Njombe wakati wa uzinduzi wa Saccos ya Vijana Ulembwe Saccos limited ya wilayani
humo, alisema kuwa uongozi wa saccos uangalie kwa makini mchanganuo kwa lengo
la kukupisha mtu anayeweza kurejesha mkopo.
Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya kuto rejeshwa kwa mikopo
katika saccos nyingi hapa nchini kutokana na wakopaji kuto kuwa na michanganuo
sahihi wa pesa anayokopa.
“Watu wengi wamekuwa wakikopa kwa kuangaliwa mwenzake
kachukua fomu ya mkopo basi nae anachukua lakini unakuta mtu hana malengo ya
mkopo na wengine wanakopa pesa zaidi ya lengo lake na kushindwa kurejesha,”
alisema Kilasi
Alisema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa wakijiingiza
katika mikopo kwa kuiga na kujikuta wakibadilisha sehemu za kukopa kwa kulipa
madeni katika saccos za awali.
Kwa upande wao wananchi na viongozi wa Kijiji Cha Ulembwe
ambapo ndio makao makuu ya sakosi hiyo wamewataka vijana kujiunga katika
vikundi mbalimbali zikiwemo sakosi ili kuweza kusaidiwa na serikali katika
mikopo yake kwa vijana.
Katibu wa saccos, Nebchard Msigwa alisema kuwa kupitia hapo
wataweza kuwakopisha vijana hasa zile pesa za serikali zilizo tengwa kwajili ya
vijana na wanawake kwa kuwa hapo ni sehemu ambayo ni salama na inaaminika kama
anavyo eleza.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ulembwe, Peter Luhasi aliwataka
wananchi hao waliojiunga katika saccos hiyo na kupata mkopo wa pembejeo za
wakati wa uzinduzi wakawe mabarozi wazuri kwa wenzao ili nao wajiunge.
Naye diwani wa kata hiyo, Agneta Mpangile alipongeza juhudi
za wananchi waliojiunga na saccos hiyo na kunufaika na matunda ya pesa wanazo
weka kwa kupata mkopo wa pembejeo.
Kwam muda wa mioezi sita wamefanikiwa kuweka pesa zaidi ya
milioni 4 hivyo wakiendelea hivyo wanaweza kufika mbali na kuinua uchimi wao
kwa kukopeshana.
Aidha mkuu wa chuo cha maendeleo ya Wananchi, Yohanes
Chongolo alihimiza wananchi kujitokeza kujiunga ili kuunganisha nguvu katika
saccos kwa kuwa kwa mwananchi wa sasa bila kukopa hawezi kufanya maendeleo thabiti
lakini wakiunganisha mitaji yao wataendelea kwa kukopeshana.