JESHI la polisi mkoani Njombe limelalamikiwa kufanya uvamizi
katika kambi wafanyakazi wa kiwanda cha chai cha Kibena cha mkoani humo na
kuwachalaza viboko wafanyakazi walio kuwa wamelala na pamoja na familia zao na
kufanya unyanganyi wa simu huku wengine wakiwakuta wakiwa uchi.
Wakizungumza na Elimtaa kwa nyakati tofauti wafanyakazi wa
kiwanda hicho wamesema kuwa jeshi la Polisi lilivamia katika kambi zao ambapo wanaishi
na familia zao na kuvunja milango huku wakitoa amri za kuwataka watoke nje na
kuwachalaza viboko na kuwapa adhabu mbalimbali za kuruka vichura bila kujali ni
mfanyakazia ama ni mwanafamilia wa mfanyakazi.
Mmoja wa wahanga wa kadhia hiyo Vumilia Ngewe alisema kuwa
yeye alitoka kazini saa 12:00 asubuhi ambapo aliingia kazini hapo usiku wa
kuamkia asubuhi ya juzi.
Akisimulia mkasa huo kwa shida kutokana na kipigo alicho
kipata na kunyanganywa simu yake alisema; “Asikari walikuja usiku majira ya saa
9 wakati tupo kazini walitukuta sisi tunataka kutoka kwa sababu boila ilikuwa
imezima kitu kilicho tulazimu kuzima mitambo kiwandani lakini walipo fika
ofisini walituamuru tuwashe mashine na tuendelee na kazi huku wengine walioko
nje ambao walikuja kwajili ya kutupokea wengine wakipewa adhabu na wengune
wakiwekwa pembeni,” alisema Ngewe
Alisema kuwa Polisi walipo fika katika kiwanda hiki walitoa
adhabu kwa baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwepo kiwandani hapo bila ya
kuuliza kunanini huku maswaliyao yakiwa ni kujua kwa kila mtu ratiba yake ya
kuja kazini.
Ngewe alisema kuwa yeye na wenzake ulipo fika mda wa kutoka
kazini walitoka na wakati wakutoka polisi waiingia kiwandani humo na kumwambia
kiongizo wao katika zamu yao na kumwambia umefunga vizuri ofisi kisha wakaona
walio kuwa wanatakiwa kuingia zamu majira ya saa 12:00 asubuhi wakiwa wanalia
na kusema wenzao wanaadhibiwa kwa kupigwa na kugalagazwa katika tope.
Alisema walipo fika katika geti la kiwanda hicho walikuta
wenzao wakipigwa huku wengine wakiwa hawatambuliki nyuso zao kwa kuwa walikuwa
wametapakaa tope usoni na kupigwa ambapo walikuwa na majeraha mbalimbali na wao
kuamurishwa kwenda katika kambi zao wanazo ishi.
Alisema kuwa chanzo cha polisi kufika katika kiwanda hicho
ni mabosi wao ambao walitakiwa kukaa nao kikao majira ya saa 3:00 asubuhi, na
kubadirisha tangazo la kikao hicho na kuwa saa 9:00 kitakaliwa kikao hicho
kinyume na makubaliana yao katika kikao chao cha tarehe 3 mwezi huu ambapo
kamanda wa polisi aliwataka siku hiyo kuto fanyakazi na kuwa itakuw ani siku ya
kikao.
“Kikao chetu kilitakiwa kukaliwa leo (juzi) saa 3 asubuhiu
na ndio maana wenzetu wengine wamewahi kuja hapa kiwandani ili kuwazuia wengine
ambao walitakiwa kuingia asubuhi kuwa kuwa kamanda wa polisi alivyo kuja
Januari tatu katika mkutano wetu na kutuambia siku ya leo hakutakuwa na kazi
yoyoto na kazi zitaendelea baada ya kikao, ratiba ya mkutano kuwa saa 9
imebadilishwa wakati wengine walikuwa hawafahamu” alisema Ngewe.
Aidha mama huyo alisema kuwa baada ya kwenda nyumbani katika
hizo kambi zao alikumbwa na kizazaa baada ya kusikia king’ora cha gari la
polisi kikiingia katika kambi zao na kuanza kuwatoa ndani kwa amri kuwa watoeni
waume zenu na kuingia ndani kwa kuvunja milango.
Alisema kuwa yeye kwakua alikuwa ndiyo anatoka kazini
aliamuliwa kufungua mlango na kuwaambia kuwa
alikuwa anatoka kuoga alisema polisi walivunja mlango na kumkuta akiwa
uchi na kumwambia awaonyeshe mmewe na kuanza kutafuta kama kuna mtu mwingine
katika chumba hicho bila mafanikio huku mama huyo akiwa uchi na kisha kuchukua
simu yake aliyo kuwa anaitumia kama taa wakati akivaa.
Alisema kuwa polisi walifanya hivyo katika kambi nzima na
kuwachalaza viboko wakazi wa kambi hizo bila kujali kuna watoto ama lah na
baada ya kuuliza simu yake polisi walikana kuichukua simu hiyo na mkuu wa
kikosi kilicho kuwa kikitekeleza zoezi hilo alisema kuwa askali wake sio wezi
licha ya mama hiyo baada ya masaa kadhaa kupita kupigiwa simu na kupitia simu
yake kwa mdogo wake na kuambia wa unajua unaongia na nanani kisha simu hiyo
kuzimwa.
Naye mmoja wa waathilika wa tukio hilo ambaye ni mke wa
mfanyakazi kiwandani hapo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa
alisikia mabomu yakipigwa kiwandani wakati yeye akiwa kambini kwake na kuwa aliamua
kumuuliza mumewe kilicho tokea kazini kwa kuwa alikuwa kambini.
Alisema mumewe alimwambia kuwa hali sio shwari kazini na
kuwa alikuwa na ratiba ya kupeleka chai kiwandani hao aliambiwa asiende na
baada ya muda fupi alisikia mabomu mengine yakipigwa na kuwa baada ya hapo
alisikia king’ora kikilia kuelekea katika kambi yao na kisha kusikia sauti
zikiwataka kutoka nje huku nyumba za majilani zake zikuvunjwa milango na
kusikiks sauti za vilio.
Alisema kuwa yeye katika nyumba yake alikuwa ametembelewa na
nduguzake alivunjiwa mlango na kuanza kuchapwa viboko na askali hao huku
wakiondoka na wanaume wote walio kuwa katika kambi hizo na kuwa wakati
wakiondoka walikuwa wakiuliza majina ya wale wanaume na kuwatenga huku
wakilinganisha na kmajina walikunayonayo.
Mmoja wa wafanyakazi ambaye alikutwa amelala kambini kwake
kutokana na homa liliyo kuwa inamsumbua alisema
kuwa aliadhibiwa na askari hao kwa kuchapwa viboko na kuamuliwa yeye na
wenzake kutembelea tumbo.
Kwa upande wa chama cha wafanyakazi sekt ya mashambani (Tpau)
kanda ya Iringa inayo shughulikia na mkoa wa Njombe, Katibu wake, Deus Magesa
alisema kuwa chama hicho kinalaani kitendo kilicho fanyw ana jeshi la polisi
kwa kuwanyanyasa wafanyakazi hao kwa kuwa nguvu waliyo itumia haikupasha
kutumika.
Alisema kuwa kuwa kulikuwa na taarifa za awali kuwa
kungekuwa na kikao cha wafanyakazi yote kiwandani hayo na uongozi wa kiwanda,
na kuwa taarifa hizo ziribadilishwa Januari 23 siku tatu kabla ya tukio na
wafanyakazi walio kuwa wamekuja asuhi siku ya tukio walikuwa hawana taarifa za
mabadiliko ya mkutano huo.
Alisema kuwa alisema kuwa wafanyakazia hao hawakuja
kiwandani hapo asubuki kwa lengo la kufanya mgomo lakini kulikuwa na
mkanganyiko wa taarifa za kikao hicho, na kuwa kitendo kilicho fanywa na jeshi
la polisi hakikuwa sahihi.
Alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wamepigwa
walikuwa wamekuja kiwandani hapo ulikuwa ni mda wao wa kazi, na wengine
walikuja hapo wakiwa na taarifa za mkutano wa saa 3 asubuhi, alisema baada ya
kuzungumza na uongozi ulisema kuwa uliita polisi baada ya kuona baadhi ya
matangazo ya mkutano kuwa yameondolewa.
Kitendo hiki kinatakiwa kupingwa na jamii yote na jeshi la
pilisi sio sehemu ya kutatua matatizo ya wafanyakazi na kuwa kwa mujibu wa
sheria ya wafanyakazi Polisi watahusika poale tu patakapo kuwa na uvunjifu wa
amani mahara pa kazi lakini kiwandani hapa hapakuw ana uvunjifu wa amani.
“Polisi watahusika pale tu patakapo kuwa na uvunjifu wa
amani, lakini wafanyakazi walikuwa nje ya geti walikuwa wamekaa kwa hiyo
kulikuwa na amani polisi wamewapiga wafanyakazi na wengine walikuwa wamelala,
na wengine kuibiwa pesa na mfanyakazi huyo ameeleza mbele ya uongozi
amechukuliwa shilingi laki 3 (300,000) ambazo anafanyia biashara ya M-pesa na
mwingine amepigwa akiwa uchi wakati akibadilisha nguo wamemfuata nyumbani
kwake,” alisema Magesa.
Alisema kuwa wamekaa na uongozi wa kiwanda kikao ambacho
kimedumu kwa zaidi ya masaa manne ambapo anamesema kuwa walizungumza na uongozi
wa kiwanda na kuwa wamefikia maamuzi ya kuwa mkutano baina ya uongozi na
wafanyakazi utakuwa Februari 23, na uongozi umekubali kuwa waliwaita polisi
lakini hawakuwataka watumie nguvu waliyo itumia.
“Uongozi tulipo uuliza kwanini ulitumia guvu hiyo ulisema
kuwa haukuliambia jeshi hilo litumie nguvu hiyo na kuwa uongozi unashanga kwa
kilew kilichotokea, tumeutaka uongozi kuwaachia wale walio shikiliwa na jeshi
la Polisi na wataendelea na kazi hadi watakapo kaa kikao chao na wale walio
pata madhara tutaibana menejimenti kuhakikisha inawafidia,” aliongeza Magesa.
Waandishi wa hanari walifika katika ofisi ya uongozi wa
kiwanda hicho kutaka kujua mengi zaidi kuhusiana na kilichotokea na maamuzi
waliyo yafikia lakini meneja wa kiwanda hicho Miraji Gembe alisema kuwa hayupo
tayari kuzungumza chohote kwa kuwa anashughulika na watu wa usalama (Polisi).
Kwa upande wake kaimu
kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Lucy Mwakafywila alisema kuwa wanawashikilia
wafanyakazi 14 wa kiwanda cha chai wanashikiliwa kufuatia tatizo
hilo kwaajili ya uchunguzi huku wafanyakazi 26
waliokamatwa juzi wakiachiwa.
Kamanda Mwakafulila alisema
kuwa polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la
kuwatawanya wafanyakazi ambao hawakupaswa kuingia kazini ambapo anasema
kwa taarifa silizo mfikia hakuna mtu yaliye pigwa tofauti na kile Elimtaa
ilichojionea katika eneo la tukio.