CHAMA cha mapindizi CCM mkoa wa Njombe kimesema kuwa
kitakata majina ya wote watakao cheza lafu wakati wa uchukuaji wa fomu za
nyadhifa tatu zilizoanza kutolewa julai 15 mwaka huu, nchi nzima kama walivyo
fanyiwa viongozi wa ngazi ya kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani humo katibu wa
chama hicho mkoa wa Njombe Hosea Mpagike alisema kuwa fomu hizo zinaaza
kutolewa katika ofisi mbalimbali za CCM na kuonya watakao anza kupiga kampeni
mapema na watakao vunga taratibu na kanuni.
Mpagike alisema kuwa fomu hizo zitaanza kutolewa Julai 15
mwaka huu na kufikia ukomo Julai 19 ambapo kampeni zitaanza rasim katika maeneo
mbalimbali na kutafuta watu watakao waopigia kura huku kukiwa hakuna kipengele
cha kutafuta wadhamini kama ilivyo kuwa katika nafasi ya urais.
“Fomu zinaanza kutolewa leo (jana) na kufika ukomo tarehe 19
na kampeni zitaanza rasm julai 20 mpaka julai 31 na uchaguzi ndani ya chama
kufanyika Augosti mosi, na zitatolewa katika ofisi za kata kwa udiwani na
ubunge katika ofisi za wilaya,” alisema Mpageke.
Alisema kuwa wanachama wanao chukua fomu wawe makini katika
suala la kupiga kampeni mapema na kuvunja kanuni za chama majina yao yatakatwa
hawato muonea huruma mtu kuwa huli.
“Kwa atakaye piga kampeni mapema na kuvunja kanuni jina lake
litakatwa tu hatutakuwa na huruma na mtu kwa sababu katiba ya chama hairuhusu
kitendo cha kupiga kampeni kabla ya kuruhusiwa,” alisema Mpagike.
Aidha mpagike alisema kuwa baada ya kupitishwa majina ya
wagombea wa Ubunge yatapitishwa na kamati kuu ya CCM NEC ambapo majina yatakayo
letwa na chama hicho yataangaliwa kama
watu hao wanakubalika kwao.
Akisoma ratiba ya utoaji wa form Mpagike amesema kuwa fomu
za udiwani zitatolewa katika ofisi za makatibu kata wa CCM na kwa ofisi za
ubunge zitatolewa katika ofisi za wilaya, na kwa wagombea udiwani nafasi ya
viti maalumu zitatolewa katika ofisi ya CCM Wilaya na ubunge viti maalumu zitatolewa
katika ofisi ya UWT mkoa.