WANANCHI wa vijiji vitatu katika kata ya Ramadhani mkoani
Njombe wamepinga ujio wa kampeni ya Uchimbaji wa madini katika vijiji vyao
ambayo iliitisha mkutano na wananchi hao kwa mara ya kwanza na wanakijiji hao
kwa lengo la kuwaomba kutoa maamuzi ya kuwapatia eneo hilo kwaajili ya
kufunguliwa mgodi wa Dhahabu.
Hatua hiyo ilikuja
juzi baada ya kampuni ya Noravia Gold iliyoitisha mkutano na wananchi
kwa lengo la kuwataarifu juu ya upatikanaji wa madini ya Dhahabu katika vijiji
vya Mgodechi, Igagala na Wikichi, ambapo lengo la mkutano huo ikiwa ni kupata
maamuzi ya wananchi juu ya kuanza kuchimba madini katika vijiji hivyo.
Katika mkutano huo uliohudhuliwa na wataalamu wa maliasili,
ardhi na afisa Maendeleo kutoka halmashauri ya mji Njombe, huku mkutano ukiwa
ni wa kuwataka wananchi waseme wanataka wafanyiwe nini na mgodi huo ili
wauruhusu kuanza kufanya kazi, wakifishwa madhara baada ya kuanza kuchimbwa
madini katika eneo hilo.
Wananchi wa vijiji hivyo walivuruga mkutano huo kwa malengo
ya kutaka mkutano wao kwanza kufanyika kabla ya kukutana na wawekezaji hao
ambao watatakiwa kuja kukaa na wananchi baada ya mkutano wao kufanyika na
kujadiliana wakiwa peke yao.
Walisema kuwa hawajapendezwa na kidendo cha serikali yao kuto
pewa taarifa mapema juu ya ujio wa wageni hao wa mgodi huku wakitupiwa lawama
ofisi ya Mkurugenzi kuwaruhusu watafiti kufanya utafiti bila wenyeji wa vijiji
hivyo kupewa taarifa.
Mmoja wa wakati hao na aliyekuwa Diwani wa kata ya Ramadhani,
Alfred Luvanda alisikika akitoa sauti ya kulalamika kwa kupinga kuwapo kwa
mkutano huo na kuanza kuwaandikia majina wananchi kabla ya wananchi hawajajua
nini malengo ya mkutano.
Alisema kuwa haiwezekani wananchi wakaanza kuandikisha majina
katika fomu ambazo hawajapewa maelekezo ya kutosha na bado hawajakubali kutoa
eeo hilo na kuwa mgodi wa madini.
Aidha Abubakar Msigwa mjumbe wa serikali ya kijiji cha
Mgodechi alisema kuwa haiwezekani wawekezaji hawa wakawa wanaeleza tu juu ya
kutoa ajira kwa wakazi wa vijiji hivyo na lakini hawaelezi madhala yatakayo
jitokeza baada ya kuanza kuchimba madini.
Alisema kuwa wananchi wa vijiji hivyo wanategemea maeneo hayo
kwa kilimo, na maisha yao yote haitawezekana kuwahalibia maeneo wanayo tegemeo
kwa kilimo kwa kulipwa fidia inatakiwa wawekezaji waje na sela itakayo
wawezesha wanakijiji kuwa na maisha bora kwa maisha yao yote rasivyo
haiwezekani.
“Wananchi wa vijiji hivi vitatu wataenda wapi wakati shughuli
za migodi zinaendelea kwa kuwa tumeshuhudia maeneo mbalimbali kukutoea migogolo
kama Mtwala ni kutokana na kuto kuw na kauli nzuri zinazo wawezesha wakazi
kunufaika licha ya serikali kunufaiki,” alisema Msigwa na kuongeza
“Napenda nchi yangu kupiga hauta ya Maendeleo lakini
haiwezekani kujengwa barabara na wananchi kufa basi nani atakaye furahia
Maendeleo hayo kwa kuwa kunanchi kunatokea vita kutokana na mali zinazochimbwa
arhini na wananchi kuto nufaika,” aliongeza
Mkutano huo baina ya Noravia na wanavijiji hao ulivinjika
huku watendaji kutoka halmashauri ya mji Njombe wakisema kuwa wanakubaliana na
kauli za wananchi ya kusuburi wananchi waitishe mikutano yao ili wamewe
kukubaliana wao wenyewe ndipo wawaite wawekezaji.
Ernest Ngaponda afisa kilimo halmashauri ya mji alisema kuwa
yeye anawaongoza wananchi katika kilimo hawezi kukubali kirahisi wananchi
kuhalibiuwa mazingira yao ya kilimi eti kwasababu ya Uchimbaji wa madini na
kuwataka wananchi kukaakatika mikutano yao kujadili madhara na faida endelevu
kwa wakazi wa eneo hilo.
Awali wakijitambulika wawekezaji hao kutoka kampuni ya Noravia
walisema kuwa wamekuja kwaajili ya kutaka kupata maoni ya wananchi juu ya nini
wawafanyie watakapo anza kuchimba madini na kuwaeleza kuwa wamefanya utafiti wa
madini katika vijiji hivyo na kubaini mkuwa kuna madini.
Mwanaseria wa serikali aliyekuja chini ya kampuni hiyo ya
madini George Stevin alisema kuwa mkutsno ho ulikuwa kwaajili ya kutoa maamuzi
juu ya mgodi wa madini na kusema kuwa kampuni hiyo ipo katika vijiji hivyo
tangu mwaka 2013 mwaka huu huku ikifanya utafiti na kugundua kuna madini mengi
chini ya ardhi na madini yenye thamani ni dhahabu.
Alisema kuwa Noravia iliomba fulsa ya kupata maoni na ruhusa
ya kupata nafasi ya kuchima madini ambapo kupitia mkutano huo wananchi wangeipa
nafasi kampuni hiyo kupata kibali cha Uchimbaji wa madini na mpaka mwisho wa
mkutano wananchi wataka kupewa muda wa kufanyamaamuzi.