WAKAZI wa mkoa wa Njombe wamesema kuwa wanataka mbunge
atakaye kuwa na ofisi Mkoani humo ili kupeleka matatizo yao wanapo kuwa na
tatizo linalo mhusu mbunge.
Wito huo umetolewa na wakazi wa mkoa wa Njombe wakati Wabunge
wakiendele na zoezi la kuchukua fomu nchini kote kwa lengo la kuwa na ofisi ya
kufikisha mawazo yao, matatizo na kelo zao katika kila jimbo.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti wakazi wa mkoa wa Njombe wamesema kuwa hawajawahi hubahatika
kuwa na ofisi ya mbunge ambako wangefika kuto shida zao hatakama mbunge hayupo
kutoa kwa katibu wa mbunge.
Mmoja wa kakazi wa mkoa wa Njombe, Enock Mwangongolwa
alisema kuwa wanataka mbunge atakaye kuja aweke ofisi ya mbunge ambako wananchi watawasilisha matatizo yao katika
ofisi yao ya mbunge.
Mwangongolwa alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Njombe wakekuwa
wakishindwa kutoa matatizo yao kwa mbunge kwa kuwa hakukuwahi kuwa na ofisi ya
mbunge.
Aidha Erick Sanga alisema kuwa amezunguka mikoa mingi hapa
nchini ameona ofisi ya mbunge lakini katika mkoa wa Njombe hajaona ofisi ya
mbunge hivyo anamba mbunge atakaye pita kwa chama chochote awe na ofisi ya
mbunge ili wananchi wawe na ofisi yao ya kuwasilisha matatizo yao.
Alisema kuwa atahakikisha kuwa atahakikisha kuwa yeye akiwa
bungeni watu wanapata huduma katika ofisi ya mbunge na kuwa ofisi ya mbunge
haiwi katika ofisi ya chama na kuwa ina wanyima uhuru Wananchi wa kupata huduma
stahiki.
Alisema kuwa hatapendezewa na kutokuwapo kwa ofisi ya mbunge
na atashawishi halmashauri kutoa kiwanja kwaajili ya ofisi ya mbunge.
Aliongeza kuwa atahakikisha kuwa anasimamia haki za wananchi
hasa za kufanya pesa za jimbo kufanya kazi ya Maendeleo ya miundombinu ya
barabara kwa lengo la kupandisha thamani ya madhao ya wananchi.
Akitoa taarifa kwa mwenyekiti wa CCM mkoa, Deo Sanga waliochukuo
fomu kwa majimbo matatu ya wilaya ya Njombe mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo
Sadakati Kimati alisema kuwa mpaka kufiukia julai 17 mwishoni mwa wiki iliyopita
kulikuwa na watu 18 huku jimbo la Makambako la mwenyekiti wa, mkoa likiwa na
wagombea wawili wkiwemo na mwenyekiti mwenyewe.
Alisema kuwa kwa wilaya yake kuna watu wengi walio hamasika
kujitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi kwa kuwa wamejipina na kuona
wanatosha kuwaongoza wananjombe tofauti na mika ya nyuma ambapo kulikuwa na
watu wachache wakijitokeza.
Aidha Kimati alitoa onyo kwa wagombea kutoa anza kuchapisha
mabango, Karenda na vipeperusi mpaka watakapo ruhusiwa kuanza kampeni na kuwa
kufanya hivyo ni kinyume cha kanuni za chama hicho.