Vijiji jirani na chanzo kupatiwa maji




 Jah People akizungumza na wananchi
 Jah People na Amos Makalla wakizindua mradi wa maji 

Makala akizungumza na wananchi baada ya kuzindua
NAIBU waziri wa maji Amos Makalla amesema kuwa serikali inatarajia kupeleka maji katika viojiji vyote ambavyo vipo katika vyanzo vyamaji na havina huduma hiyo hapa nchini kwa lengo la kuhamasika kuendelea kulinda vyanzo hivyo.

Alisema kuwa Wizara ya Maji inampango wa kuhakikisha vijiji vyote hapa nchini vinapatiwa maji ili kuimarisha ulinzi wa vyanzo hivyo vya maji na kuwa miradi hiyo kuwa ya kudumu.

Alisema kuwa kijiji cha Upami na Ilengititu havita ishia kulinda chanzo cha maji kwaajili ya vijiji vingine navyo kitapatiwa maji na kuendelea kulinda chanzo cha maji kwa kuendelea kunufaika na maji.

Makalla aliyasema hayo baada ya kuombwa kukipatia maji kijiji hicho na mbunge wa Njombe Kaskazini Deo Sanga, maarufu kwa jina la Jar People kuomba wananchi walioko karibu na chanzo hicho cha maji kwa kuwa wao wapo jirani na mradi huo na kuona wenzao wa kata nyingine wakinufaika na maji.

Aidha makalla amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombini ya maji na kuhakikisha mradi huo unakuwa wakudumu na kutumiwa na kizazi cha sasa na kijacho hivyo amewaahidi wananchi hao kuwa mradi huo utakamilika haraka iwezekanavyo na kuanza kufurahia matumizi ya maji.

Awali akizungumza katika mkutano wa hadhara mbunge Sanga alisema kuwa tangu nchi ipate uhuru vijiji vya kata ya Kifume  havijawahi kupata maji na sasa mwaka huu wananchi hao wanafurahia kupata maji, na kuachana na shughuri za kuhangaikia maji na kufanya shughuli za kimaendeleo.