Watoto wenye matatizo ya kuona mbali (Uoni Hafifu) wapatiwa vifaa mbalimbali (Under The Same Sun)







WATOTO walio na uoni hafifu wamepa  msaada wa  vifaa vitakavyo wasaidia kuona vizuri wakiwa darasani pamoja na kofia na miwani kwa watoto wenye ualbino katika shule ya msingi Kibeni inayo wafundisha  watoto wenye mahitaji maalumi mkoani Njombe.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa  juzi  na shirika la Under the Same Sun pamoja kampuni ya Tanganyika Wattle (Tanwat) ya mkoani Njombe ambapo watoto hao wamesema kuwa msaada huo utawasaida kuwaondoa na matatizo ya kutazama kwa shida wanapo soma ubaoni na wakiwa wanajisomea.

Mmoja wa watoto hao ambaye anauoni hafifu Julius Liwali, alisema kuwa msaada huo utakuwa mi msaada mkubwa katika masomo yao na unawaongezea kiwango cha ufauru darasani kwa kuwa watakuwa wakisoma kwa urahisi.

Alisema kuwa wadau wengine wasisite kuja shuleni kwao kutoa misaada ambayo itakuwa ni msaada katika masomo yao na watakuwa ni wanafunzi wengine shuleni hapo.

Rehema Nziku ambaye ana Ualbino alisema kuwa vifaa walivyo patiwa kama stendi ya meza  ambayo itawasaidia kuwaodoa na matatizo ya kuugua mgongo na shingo wakati wanasoma kutokana na kuinama chini sana wakati wakisoma.

Stendi ya meza, miwani, Kofia, pamoja na lensi ya kusomea wamepatiwa wanafunzi wa shule ya msingi Kibena ambayo inahudumia watoto wenye mahitaji maalumu kama walemvu wa macho, uoni hafifi, na albino.

Akikabidhi vifaa hivyo mkurugenzi wa tasisi ya under the same Sun Vick Ntetema alimsema kuwa kampuni ya TANWAT imekuwa kampuni ya kwanza Tanzania kubuni stendi za Meza kwaajili ya kusomea watoto wenye uoni hafifi wanapokuwa Darasani.

Alisema kuwa stendi za meza 100 ni kati ya meza 500 ambazo zinahijajika kwa kuwa sasa ambazo zinatakwenda kwa watoto wenye uoni hafifu kanda ya ziwa huku wanafunzi wa Shule hiyo wakiwa wamekabidhiwa miza tano kwaajili ya kujifunzia.


Hata hivyo mkurugenzi wa mawasiliano na fedha kampuni ya TANWAT  Edmund Munubi alisema kuwa wamekuwa wakisaidia jamii inayo wazunguka na stendi hizo ni moja ya misaada ambayo wamekuwa wakiisaidia jamii inayo wazinguka kiwanda.