CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Njombe kimesema
hakikubaliani na hatua iliyo yanywa na bunge ya kuwafukuza bungeni Wabunge wa
kambi ya Upinzani na wanao unda ukawa kwa kupinga hati ya dharula katika sera
ya gesi na mafuta.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kutangaza nia ya
kuwania jimbo la Njombe kusini linaloshikiliwa na Spika wa bunge la Tanzania,
mbunge Anna Makinda, Emmanuel Filangali,
mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Njombe Faki Lulandala amesema kuwa Chadema
haikubaliani na kitendo hicho kwa kuwa sera hiyo ina maslahi makubwa kwa
wananchi hivyo haipaswi kupelekwa haraka.
Lulandala ambaye pia anatangaza nia ya kuwania jimbo la
Njombe kusini amesema kuwa anashangaa kuona suala hilo mihumu kwa uchumi wa
Watanzania kupelekwa bungeni kwa hati ya dharula wakati suala hilo
likitengenezwa kwa utulivu kwa kuzipitia vipengele vilivyomo katika sera
linaweza kubadilisha kilimo, na kuboresha mishahara ya watumishi Chadema mkoa wa
Njombe hawakubaliani.
Aidha mtiania kuwani ubunge wa chama hicho jimbo la Njombe
kusini Emmanuel Filangali amesema kuwa akipitishwa na chama chake na kuwa
mbunge atahakikisha uchumi wa mkoa wanjombe unakuwa kwa kusimania pesa
zinazoletwa kwaajili ya mfuko wa jimbo.
Amesema kuwa atasimamia Maendeleo vijijini na kuhakikisha
vijana wa vijijini hawakimbilii mjini na kuhakikisha makusanyiko wa watu
vijijini unakuwa kama zamani kwa kuhakikisha mazingira yanawawezesha vijana
kujiajili huko.
Amesema kuwa anatamani Chadema kuchukua jimbo hilo lakini
nafsi yake inatamani yeye kuwa mwakilishi wa wakazi wa jimbo hilo bungeni.