VIONE VITU LIVILYO MTIA WASIWASI MSAMBICHAKA MGOMBEA UBUNGE LUDEWA WA CHADEMA

MGOMBEA wa ubunge jimbo la Ludewa kupitia Chadema anawasiwasi wa matokeo yaliyotangazwa kutokana na sababu mbili alizo zitaja kuwa huenda lilipunguza kura na kufanya uchaguzi kuwa sio wa huru.

Mgombea huyo Batromayo Msambichaka alisema kuwa sababu ambazo zinamfanya kuwa na wasiwasi na matokeo ni pamoja na baadhi ya mawakala walio wateua kukataliwa na vuruguzilizo tokea usiku wa kuamukia uchaguzi.

Msambichaka ambaye kura zake hazikutosha katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Ludewa, kwa kupata kura 7,956 dhidi ya mbunge mteulia wa CCM Deo Ngalawa aliye pata kura 23861 na kutangazwa mshindi.

Alisema kuwa wakati wa kupelewa mawakala kwa msimamizi wa uchaguzi baadhi yao walikataliwa kushiriki kusimamia uchaguzi huo hiyo anasema kuwa ni moja ya sababu ambayo huenda imempunguzia kura katika uchaguzi huo.

Alisema kuwa “Tulipeleka mawakala kwa msimamizi wa uchaguzi ili awathibitishe kuwa mawakala wangu katika uchaguzi huo lakini walikataliwa kwa kigezo walikuwa wametoka mbali wakati hao ndio chama kiliwasimamisha,”

Alisemam kuwa mbali na kuwapo kwa pingamizi la mawakala wa chama  hicho katika uchaguzi pia chama hicho siku moja kabla ya uchaguzi wafuasi wake walipigwa na wafuasi wanao daiwa kuwa ni wa chama cha mapinduzi.

“Usiku wa kuamukia siku ya uchaguzi wanachama wangu walivamiwa na wanachama wa CCM na kupigwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya misheni ya Lugalawa hii nayo ni sababu inayo sema kuwa uchaguzi huu siku lidhika nao,” alisema Msambichaka.

Msambichaka alisema kuwa vijana watatu wauasi wa Chadema walivamiwa na Wauasi wa CCM na kusema kuwa wauasi saba wa CCM walishikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.

Kushusi kukubari ama kukataa matokeo alisema kua anashauriana na wiongozi wa chama hicho na atatoa maamuzi ya kukubali ama kukataa matokeo.

Hata hivyo Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Wilbrod Mutafungwa alithibitisha kuwakamata watu saba wanao daiwa kuwa ni wafuasi wa CCM siku ya Jumapili kuhusisha na tukio usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura.

Kuhusiana na kuzuiwa kwa mawakala wa chama hicho msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Ludewa, William Waziri alisema kuwa wakala wa anatakiwa kutoka katika eneo la jimbo la uchaguzi na sio nje ya jimbo hilo suala hilo lipo kisheria.
Msambichaga Bathromeo wa Chadema alikuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Ludewa