WANANCHI na wafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa wamesema kuwa wanaimani
na ujio wa Waziri mstaafu katika Umoja wao kwa kuwa amekuwa kuongeza nguvu ya kuingoa CCM madarakani.
na ujio wa Waziri mstaafu katika Umoja wao kwa kuwa amekuwa kuongeza nguvu ya kuingoa CCM madarakani.
Akizungumzia Ujio wa Lowassa katika umoja huo Diwani wa Chadema kata ya Njombe, Agrey Mtambo amesema kuwa Ukawa hauna nongwa nae na kuwa mtu akikili hadharani kuachana na uovu haina shida.
Amesema kuwa ujio wake unakuja kuipa nguvu Chadema kupambana na CCM ambayo imekuwa ikiwaumiza kichwa kuiondoa madarakani.
Mtambo amesema kuwa anawakaribisha na watu wengine kujiunga na Ukawa ili wasaidie kuleta mabadiliko ya kuondoa chama kinacho wakandamiza watanzania.
Amesema kuwa haina shida kuhamia chama hicho na ni faraja kwa kwa kuwa ujio wake unawaongezea hatua moja kuelekea Ikulu.
Mtambo ameongeza kuwa kuhusu Lowassa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais hilo hawezi kulizungumzia kwa kuwa bado haja chukua fomu.
Aidha kwa upande wake Hitram amesema kuwa kuhamia kwa Lowasa hakuna shida katika umoja wa ukawa na hiyo itawapa nguvu ya kuiondoa madarakani CCM.