JUMUIYA ya wafanyabiashara hapa nchini imesema kuwa itahakikisha kuwa inakaa na wagombea wa urais hapa nchini bila kujali wanatoka chama kipi cha siasa na kutaka kujua kama atawasaidia ili wamuingize madarakani na kumjazisha mkataba kaajili ya kumfuatilia kama atatekeleza waliyo kubaliana nayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua ofisi ya jumuiya ya wafanyajiashara mkoani Njombe mwenyeki wa jumuiya hiyo taifa Jonson Minja jana amesema kuwa watawakalisha wagombea wa urais ili kujua atawafanyia nini na ili wamchague kuwa rais.
Amesema kuwa mkutano huo utakao jumuisha wafanyabiashara wote nchini utafanyika jijini Dar Es Salaam, na kuwashirikisha wagombea wote ili wajue watafanyiwa nini baada ya yeye kuingia madarakani.
Amesema kuwa watakapo ingia katika mkutano huo watakiwa hawajui na hawana maamuzi maamuzi yao yatakuja baada ya kuhakikishiwa kuwa watafanyiwa vile wanavyo hitaji ili kuujenga uchumi wao.
Amesema kuwa baada ya mkutano huo na wagombe wa urais watawajazisha mkataba wa makubariano yao na watafuatilia kwa makini kile walicho kubaliana nae ili kuinua uchumi wa wafanyabiashara.
Minja ameongeza kuwa wanapenda kulipa kodi na wanawahimiza wafanyabishara kwenda kilipa kodi kwa kuwa suala la kodi ya ongezeko kwa asilinia 100 wamelishughulikia na sasa ni asilimia 50 na kuwa wamefikia muafaka wa kuwa kodi itatakiwa kupanda kulingana na ongezeko la uchumi.
Amesema kuwa kuhusu suala la mashine za kutolea risisi za kielekroniki EFD zilizo leta mgogoro mkubwa hapa nchini serikali kwa kusirikian ana wafanyabiashara wanaendelea na mchakato wa kujifunza katika nchi za jirani huku akisema wameenda Uganda na kunanchi wanatarajia kwenda.