KAULI NANE ZA EDWARD LOWASSA WAKATI ANAJIUNGA NA CHADEMA LEO HIZI HAPA


 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.Picha na Ahmad Michuzi


Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), leo Jijini Dar na hizi ndizo kauli alizozitoa wakati wa hotuba yake

Lowassa: Namshukuru mke wangu Regina, wanangu na wanafamilia katika kipindi hiki kigumu kilichojitokeza.

Lowassa: Nawashukuru wanaCCM waliojitokeza kuniunga mkono wakati nikitafuta wadhamini.

Lowassa: Kilichotokea Dodoma, ni kupora madarakani ya kamati kuu, waswahili wanasema kubaka madaraka.


Lowassa: Chuki na roho mbaya zilitawala licha ya mimi kuwa mgombea mwenye ushawishi na anayekubali zaidi kuliko wote.

Lowassa:Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kudanganya nafsi yangu na Watanzania kuwa bado nina imani na CCM.

Lowassa: Sijakurupuka kwa uamuzi huu, nawaomba watanzania wajiunge na UKAWA katika Safari ya Matumaini.

Lowassa: Wanaoogopa kisasi wamefanya madhambi gani? Waulizeni..mimi ni Mkristo,sina kisasi..waende wakatubu kwa Mungu wao.

Lowassa: CCM Si baba yangu wala Mama yangu. Watanzania kama wameyakosa mabadiliko ndani ya CCM, basi watayapata nje ya CCM.

Related Posts