RUFAA YAKUBALIWA JINA LA MGOMBEA LALEJESHWA




MGOMBE wa nafasi ya uwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kibena kati,
Benard Konga ambaye aliwekewa pingamizi na kuenguliwa katika
kinyanganyiro hicho.
Uamuzi huo wa kamati umekuja baada ya Chama cha Demokrasia na
(Chadema) wakiongwa na diwani wa Chadema Njombe mjini, Agrey Mtambo,
kupiga kambi katika ofisi za kamati ya rufaa.
Kuanzaia majira ya saa nne wakisubili maamuzi ya kamati hiyo bila
kuondoka katika ofisi za kamati hiyo ambayo inasimamiwa na katibu
tawara wa wilaya ambapo katika ofisi hiyo kuna kaimu katibu tawala
ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya rufaa, Anna Wiketye ilitoa maamuzi
hayo majira ya saa 9:15 za alasili.

Awali katika mkutano wa Chama hicho na kamati mwenyekiti huyo, Wiketye alikili kuwa kuna makosa yalifanyika katika utoaji wa maamuzi ya awalibaada ya kusomewa baadhi ya vifungu katika sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Baada ya kukamilika kwa kikao ambacho kilidumu kwa muda wa masaa
mawili ndani ya kamati hiyo mwenyekiti wa kamati hiyo alikataa
kuzungumzia suala hilo kwa vyombo vya habari juu ya kilicho jili ndani
ya kamati hiyo na kudai kuwa yeye sio msemaji na kuwa yupo msemaji
ambaye angeweza kuzungumzia suala hiyo na kuwakabidhi rasm barua ya
kutupilia mbali pingamizi la mgombea wa mtaa wa Kibena Kati.

Wanachama hao wamepokea barua hiyo na mgombea huyo kuisoma waziwazi
katika mkutano wa hadhara katika mtaa wa kibena Kati ambako ndiko
mgombea huyo anatoka.

Aidha katika barua hiyo ambayo East Africa Radio imeishuhudia ikisomwa
katika mkutano huo imetoa ruhusa ya mgombea kugombea na hapa kama
ilivyo somwa na mgombea na anatoa lai kwa serikali,

Moja ya kosa ambalo kamati hiyo imekili kulifanya wakati wa kutoa
maamuzi yake ni kumtoa mgombea ambaye ana kadi mbili za vyama vya
siasa hakumzuii kugombea nafasi yoyote ya uongozi.


Katika chama hicho mkoa wa Njombe, kuna wagombea zaidi ya 61 walio
enguliwa ugombea baada ya kuwekewa pingamizi katika halmashauri mili
tofauti na halmashauri ya Wanging'ombe kuwa na wagombea 60 wa nafasi
ya uwenyekiti na mmoja halmashauri ya mji wa Makambako huku mmoja wa
kubena ndio huyo katengua maamuzi ya rufaa