Wananchi watahadhalishwa na viongozi wababaishaji



WANANCHI mkoni Njombe wametakiwa kuchagua viongozi waadilifu ifikapo octoba 25 mwaka huu ili waweze kupata uwakilishi mzuri badala ya kuwapa nyadhifa watu wanaotaka kujinufaisha wenyewe

Hayo yamebainishwa katika jimbo la Njombe kusini linalotawaliwa na spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda linaonekana kupata upinzani mkubwa kufuatia idadi ya wagombea kuendelea kujitokeza kutangaza nia ya kutaka kuliongoza


Akitangaza nia mgombea wa nne kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Njombe Kusini, Rafaeli Rulandala ambaye ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Njombe katika mkutano wa hadhara na kufanya idadi ya wanao wania kugombea kwa tiketi ya chama hicho kufikia 11 huku chama cha Mapinduzi wakifikia 4.


Rulandala amesema pamoja na idadi kubwa ya wanaowania kuteuliwa kuwania nafasi hiyo atakuwa tayari kumpa ushirikiano atakaye teuliwa kuipepersha bendera ya kwa tiketi ya Chadema ili kuhakikisha jimbo hilo linachukuliwa kutoka chama tawala

Ameeleza kuwa jamii kwa sasa inakabiliwa na changamoto nyingi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kilimo na miundombinu ambapo kama atateuliwa atavipa kipaombele



Aidha Lulandala amesindikizwa na katibu wa chama hicho mkoa wa Njombe ambaye pia ni mtangaza nia, Alatanga Nyagawa alionyesha masikitiko yake dhidi ya dhuluma kwa wananchi inayofanyika  na vingozi wa chama hicho akitolea mfano ubadhirifu katika halmashauri ya wilaya ya Njombe na hospitali ya wilaya ya Njombe


Mkutano huo wa kutangaza nia umehudhuriwa na mtangazania kutoka jimbo la Njombe kaskazini Oraph Mhema ambaye ni msemaji wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe na mjumbe wa halmashauri kuu  Chadema mkoa wa Mbeya Joseph kasambala 

Kasambala alisema kuwa wananchi wakubali kuwa mabadiliko hayata kuja kama wataendelea kuchagua viongozi kana Anna Makinda hakutatokea uongozi wa chama kingine.