ZOEZI la uandikishaji
Daftari la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa kibaiolojia (BVR) umedaia
kufelisha wanafunzi katika mihani wa moka halmashauli ya wilaya ya Njombe baada
ya walimu wao kutumiwa katika zoezi hilo.
Hayo yamebainishwa katika baraza la Madiwani wa halmashauri
ya wilaya ya Njombe na Madiwani baada ya walimu wa shule za kata zao kutumika
katika zoezi la uandikishaji huku shule hizo zikiwa na walimu wachache.
Akichangia taarifa ya elimu ya kukamilisha mwaka uliopita wa
fedha hasa katika mtihani wa kujipima uwezo wa darasa la saba (Mock) Diwani wa
viti maalum kata ya Mfiliga, Salome Lugala amesema kuwa wanafunzi katika kata
yake wamefeli kutokana na walimu wa shule ya msingi Iditima walimu wote kwenda
kwenye zoezi la uandikishaji na kuacha shule zao kuwa bila walimu kwa kipindi
chote cha uandikishaji.
Amesema kuwa serikali imekuwa ikisema kuwa walimu wanapewa
motisha kwa kufanya kazi hilo lakini haiangalii madhara yanayo weza kujitokeza
baadae.
Diwani wa kata ya Igogolo Ayubu Mkane amesema kuwa serikali
inapashwa kuto tazama motishwa kwa wafanyakazi wa chini pekee itazame na
madhara kama hayo na kuwatumia wasomi walioko mitaani kwa kuwapatia fura hizo
ili nao kupata pesa kwa kuwachanganya na wafanyakazi wa serikali.
Awali akiwasiliasha taarifa ya elimu afisa elimu shule za
msingi halmashauri hiyo Frida Kayava amesema kuwa taarifa ya elimu hiyo ipo
katika sehemu tatu na imeeleza sababu za kufeli na mikakati ya huhakikisha elimu
inapanda juu.
Aidha Ahmed Maguho kaimu Mkurugenzi amesema kuwa serikali
kwa kuona matokeo hayo imeamua kuanza mikutano ya kuwakutanisha wakuu wa shule
kwa kuwapa mikakati ya kupandisha elimu katika halmashauri hiyo na kuwa
mikutano hiyo imeisha anza katika kata mbalimbali za halmashauri hizo.
Naye kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Shaibu Masasi amesema
kuwa halmashauri hiyo isijidai kuwa imejitahidi wakati haina alama ya kujani
hata mija katika ufauru kwa kuwa hakuna shule hata moja zote zina langi ya
njano kwa ufauru.
