JESHI la polisi kwa mwaka jana limefanikiwa kukusanya jumla
ya shilingi milioni 599.4 katika tozo mbalimbali za makosa ya barabarani kwa
mwaka jana na kuwa pesa hizo ni ongezeko la milioni 176 ulikinganisha na mwaka
juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe kamanda wa
polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani, wakati wa kutoa tathimini ya mwaka
mzima wa makajana kulinganisha na mwaka juzi, alisema kuwa jeshi hilo
limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi miloini 599, 400,000 kwa mwaka jana
ambapo pesa hizo ni sawa onezeko la shilingi 176.5.
Alisema kuwa mwaka juzi jeshi la pilisi lilifanikiwa
kukusanya tozo kwa makosa mbalimbali ya papo kwa hapo kwa makoya ya barabarani
jumla ya shilingi milioni 422.8 huku kwa mwaka wa jana ilikusanya shilingi
nilioni 599.4 ambapo ni sawa na ongezeko la asilinia 42.
Ngonyani alisema kuwa udhibiti wa makosa unaendelea
kuimarishwa na kuwa kwa kiwango hicho inaonyesha kuwa ni jinsi gani kwa mwaka
jana walijipanga kufuatilia makosa.
Alisema kuwa kwa mwaka huu wamejipanga kufanya ukaguzi wa
mara kwa mara katika vituo vyao mbalimbali ambapo kutakuwa na utozwaji wa faini
kwa watakao kuwa na makosa mbalimbali na kudhibiti ufanyaji wa makosa kwa
watuiaji wa vyombo vya moto.
Alisema kuwa licha ya kutumia vyombo vya habari jeshi lilo
limejipanga kutoa elimu kwa wananchi kupitia taasisi ya muungano wa jamii (Mujata)
ambayo imekuwa ikipita kutoa elimu katika mikutano mbalimbali na katisha shule
za msingi, sekondari na vyuo.