Dhamana ya dereva wa Lake Oil yatolewa

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Mkoani Njombe imetupilia mbali pingamizi la dhamana kwa watuhumiwa wa wizi wa sahani ya shaba ambao waliwekewa pingamizi hilo na upande wa mashitaja walipo pandishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo mapema januari.

Akitoa uanuzi huo wa mahakama hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi wa Njombe hakimu John Kapokolo, baada ya Januari 8 kutolewa kwa pingamizi la washitakiwa watatu na kusema mahakama ipitie pingamizi hili na kutolea uamuzi.

Pingamizi hilo liliwekwa juu ya vijana watatu, ambapo upanmashitaka ukiwa unaongozwa na wakakili wa serikali Riziki Makiku kuwawekea pingamizi kufuatia kupokelewa kwa kiapo cha pingamizi ya dhamana kwa washitakiwa hao.

Washitakiwa hao walikuwa na wakili wao Malangalila ambaye aliomba mahakama kuto weka pingamizi kwa wateja wake kwa kuwa badi hawaja kutwa na hatia na kuwa pingamizi hilo litupiliwe mbali na mahakama ambapo mahakama iliona ni vima ikapitia pingamizi hilo kwa muda ili kujilizisha.

Uamuzi wa mahakama ulitolewa juzi juu ya washitakiwa hao ambao walipandishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kuiba sahani ya shaba mali ya kampuni ya Lake Oil na mahakama kuachia wazi dhamana ya washitakiwa hao.

Hakimu Kapokolo alisema kuwa mahakama imepitia sababu za kuzuia dhamana ya washitakiwa hazima mashiko na kuwa mahakama imeachia wadhi dhamana kwa washitakiwa na kuwa washitakiwa wata pata dhamana kwa kutimiza mashariti ambayo mahakama imeyaweka.

“Washitakiwa watapata dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili kwa kila mshitakiwa na wadhamini kuwa na mali isiyo hamishina na kuwa na shilingi milioni 2 kwa kila mdhamini uamuzi huu umetolewa na mahakama leo Januari 19 na washitakiwa mtarudi mahabusu wakati mnashughulikia dhamana zenu,” alisema Hakimu Kapokolo.

Alisema kuwa mahakama iliona ni vema ikajiridhisha inapo toa maamuzi na kuwa imetupilia maombi ya upande wa mashitaka kwa kuwa washitakiwa kwa kosa lao wanahaki ya kupata dhamana iwapo watatimiza masharti ya dhamana.