Wahudumu wa baa watakiwa kujiendeleza kielimu

MKUU wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba Amewataka watu wanao fanya kazi kazi za kutoa huduma katika baa kwenda kujiendeleza ili kuimalisha elimu zao na kujikwamua na maisha kwa kupata ujila mkubwa.

Dumba ametoa wito huo wakati akizungumza na wahudumu wa baa na nyumba za kulala wageni, mkoani Njombe walio kusanywa na taasisi ya maendeleo ya vijana mkoa wa Njombe (Njombe Young Development Organization) wakati akifungua mafunzo wa wahudumu hao.

Alisema kuwa wahudumu hao ili waondoke katika mazingira magumu ya ufanyaji kazi wahakikishe kuwa ujila wanao upata wanautumia kujiendeleza kielimu ili kupanda ngazi ya ajira.

Dumba aliyasema hayo baada ya mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Aliyekuwa jasili na kusema kuwa anafanya kazi katika baa na kujiendeleza kimasomo katika mfumo wa QT (Masomo ya kujipima) huku muda wake akiugawa vizuri.

Alisema kuwa wahudumu hao waige mfano kwa mwenzao huyo kwa kujiendeleza kielimu kwa kuwa kipato wanacho kipata wakikigawa vizuri na kujipatia elimu watafanikiwa kwa kuwa wakiwa na elimu wataachana na kazi hiyo au kupanda nafasi walizo nazo.

"Kujiendeleza kwenu kielimu kutawasaidia kuongeza kupato na kujikuta mnapata ujila mkubwa kuliko vivi sasa nawaambieni elimu ni muhimu katika maisha hata kama utaendelea kufanya kazi katika kazi hizihizi ila utakuwa katika nafasi ya juu na kipato itaimarika," alisema Dumba.

Akijitambulisha katika semina hiyo Rosemary Joseph alisema kuwa yeye anafanya kazi katika Baa ya Tale mjini Njombe na anasoma QT huku akisema kuwa mda wa mchana ameachiwa na bosi wake kwenda masomoni.

Alisema akuwa ameamua kufanya hiyo kutokan ana kuona kuwa elimu yake inamfanya anyanyasike na kuto heshimiwa lakini imani yake akifanykiwa kufanya vizuri katika masomo yake atakuwa anaheshimika.

Alisema kuwa kipato anacho kipata anawekeza na kukitumia katika masomo yake, na kuwa alimepewa ruhusa ya kusoma na bosi wake na kuwa amepangiwa muda wa jioni kufanya kazi huku muda wa mchana akiutumia kwenda shule.