Kalamu za waandishi zisichukue mamlaka ya visanduku vya kura


-Kufuata maadili, miiko, sheria ndio uandishi wa habari
Na Haji Nassor, Pemba   
KUMEKUCHA Tanzania vyama vya siasa vinahaha kila kona ya nchi kuhakikisha mwisho wa siku wanaibuka na ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi.
Ni harakati za kisiasa, zinazoelezwa kuimarisha demokrasia ya kila baada ya miaka mitano, kwa wananchi kuvisogelea tena visanduku vya kura.
Ni sawa na kwamba wananchi kila miaka mitani huulizwa kwa njia ya kupiga kura iwapo wanabakia na viongozi wao wa zamani ua wanataka kuwabadilisha.
Ndio maana kila chama hujifungia kwenye vikao vizito kuhakikisha mwishi wa siku wanaibuka na mgombea mwenye sifa zote ili aingia kwenye ushindani.
Tanzania pamoja na kuwa na vyama 22 ya siasa, huwa sio vyama vyote vyenye uwezo wa kusimamisha hata wabunge, wawakilishi, madiwani na rais.
Lakini kwa vyama vilivyosimamisha wagombea kwa ngazi mbali mbali, huwa na dira, sera, ilani na mitazamo yao ambayo huyauza kwa wapigara kura.
Waandishi wa habari huwasambamba na wagombea hao kuandika habari zao na kutengeneza vipindi mbali mbali, na wengine wakisahau kufuata maadili yao.