Mlezi wa Michuano ya Kombe la Karume Cup Mama Shadya Karume akiwa na
Viongozi wa Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar (BAZA) akiwasili katika
viwanja vya Gymkhana kwa ajili ya ufunguzi wa Michuano hiyo ya 12 ya
Karume Cup tangu kuazisha.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mareheme Mzee Abeid Amani Karume Mama
Fatma Karume akisalimiana na Viongozi wa Michezo Zanzibar wakati
akiwasili katika viwanja vya Gymkhana kwa ajili ya kufungua Michuano ya
12 ya Karume Cup kwa mchezo wa Basketi Ball, akiwa mgeni rasmin wa
michuano hiyo inayoshirikisha timu 17 za Wanawake inashirikisha timu 6
na Wanaume inashirikisha timu 11.
Mama Fatma Karume akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo
Zanzibar Bi Sharifa Khamis (Shery) wakati akiwasili katika viwanja hivyo
kwa ajili ya ufunguzi wa michuano ya Karume Cup kwa mchezo wa Basketi
Ball.
Mama Fatma Karume akisalimiana na Mjuu wake Ahmeid Abeid Karume wakati
akiwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya ufunguzi wa michuano hiyo.
Washiriki wa Michuano ya Karume Cup wakiingia uwanjani kwa maandamano
kwa ajili ya Ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Mikono (Basketi Ball)
uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar
Washiriki wa Michuano ya Karume Cup wakiingia uwanjani kwa maandamano
kwa ajili ya Ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Mikono (Basketi Ball)
uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma
Karume akizundua michuano ya Mpira wa Mikono (Basket Ball) Kombe la
Karume Cup katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar, akirusha mpira kufunga
basketi wakati wa uzinduzi huo.