TIMU YA MADAKTARI BINGWA KUTOKA NCHINI CHINA WATOA HUDUMA ZA KIJAMII KATIKA KIJIJI CHA KISAUNI ZANZIBAR.



1
Dokta Gao Yun Lai akimpima presha na sukari bwana Mohd Ali, mkaazi wa Kisauni. PICHA NA ABDALLA OMAR – MAELEZO ZANZIBAR.
2
Dokta Fadhil Mohd ambae ni D0kta Dhamana Kanda ya Unguja akitoa maelezo kwa waadishi wa habari (hawapo pichani).

3
4 5

Wananchi mbalimbali wakipatiwa huduma za matibabu katika kijiji cha Kisauni Zanzibar. 
 


                   Mwashungi Tahir Maelezo-Zanzibar 

Jumla ya madaktari bingwa tisa kutoka nchini china wakishirikiyana na madaktari wa hapa Zanzibar wameweza kutoa huduma za afyakwa wananchi wa shehia ya Kisauni kwa kuwapima na kuweza kujua afya zao na kuwapatia huduma za matibabu. 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko katika shehia ya Kisauni wilaya ya Magharibi B Dr Fadhil Mohammed ambae ni dhamana ya kanda ya Unguja amesema madaktari hao wamekuja kutoa huduma za afya za jamii hapa Zanzibar. 

Amesema madaktari hao wanatoa huduma hizo vijijini kwa kila baada ya miezi mitatu wanakwenda katika kijiji chengine kwa lengo la kuwarahisishia huduma hiyo watu hao na kuwapelekea huduma hiyo katika maeneo yao. 

“Lengo ni kuwapelekea wananchi huduma hiyo karibu na maeneo yao ili waweze kupata urahisi wa kuweza kujua afya zao” alisema daktari huyo. 

Sambamba na hayo Fadhil amesema jitihada hizi ambazo zinafanywa na madaktari hao na kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ni kuweza kuimarisha huduma hiyo kupitia vijijini ili kuweza kuwapa muamko wananchi na kuweza kujitokeza kupima afya zao kwa urahisi. 

Madaktari hao bingwa ambao ni maspeshalisti wa maradhi mbalimbali wameweza kuwapima wananchi maradhi mbali mbali na kuweza kuwapatia matibabu hapo hapo bila ya usumbufu wowote. 

Maradhi wanayopima na kutoa huduma ni pamoja na ukimwi, koo, pua, meno, presha magonjwa ya moyo , ganzi, sukari na matatizo ya mkojo na maradhi mengineyo. 

Pia wanatoa huduma za akinamama za uzazi wa mpango kwa njia salama na huduma za watoto ambapo akinamama wengi wameweza kujitokeza kwa kujipatia huduma hiyo. 

Nae mratibu wa afya wa mama na mtoto Bi Fatma Ussi Yahya amesema amefurahishwa sana na akinamama wa kijiji hicho pamoja na majirani kwa kuweza kufika kwa wingi katika kujipatia na huduma hiyo. 

Pia kati ya madaktari hao bingwa Dr GAO YUNLAI amesema amefarijika sana kuona wananchi wameweza kujitokeza kwa wingi na kupima vipimo vya aina ya maradhi mbali mbali ikiwemo maradhi yasiyoambukuza ya kisuari na presha. 

Sheha wa shehia hiyo ya Kisauni Hija Suleiman Othman amewataka wananchi wake wasiidharau huduma hizi zinapofika vijijini kwani hiyo ni bahati adhimu kwa wananchi wa visiwa hivi. 

“Nimefurahi kuona wananchi wangu wameweza kuhamasika kwa kujitokeza kwa wingi kwenye huduma hizi ambazo wameletewa hapa hapa na pia huduma hizi zinatolewa bure kupitia Wizara ya Afya.” Alisema sheha huyo. 

Kwa upande wa wananchi Bi M wanajuma Omar kutoka mitondooni amesema ameweza kushiriki vizuri katika kujipatia vipimo na kuweza kujifahamu afya yake ambayo vipimo vyote alivyoima ameweza kujigundua kuwa yuko salama . 

Amewataka akinamama na akinababa kuweza kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kuweza kujitambua na kupatiwa matibabu ambapo matibabu hayo yanatolewa kwa wingi hapo hapo na kuweza kuwaambia kuwa kinga bora kuliko tiba. 

Madakatari hao ni maalum Chinese medical team wapo hapa visiwani kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi na kuweza kuwapa matibabu watu wote .