KATIBU tawara mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu ameiomba Tume ya kudhibiti Ukimwi kuhakakisha ina toa mapema takwimu ya Ukimwi ili kujua nafasi ya mkoa huo kitaifa mpaka sasa.
Ametoa kauli hiyo kwa lengo la kutaka kujua walipofikia baada ya kupambana kwa mda mrefu kudhibiti maambukidhi ya ungo njwa huo ambao una wakosesha usingizi.
Aliyabainisha hayo juzi wakati akifungua mkutano wa kujadili utekelezaji wa makumu yao ya kila siku ya kupambana ma ukimwi ambapo mkutano huo ulikusanya wadau mbalimbali Saitabahu alisema kuwa asingependa kusikia mkoa wa Njombe kuwa unaongoza kwa asilimia 14.8 kitaifa kwa maambukizi na kuwa anaomba Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Tacaids kufanya utafiti wa maambukizi ya Ukimwi ili kutoa takwimu mpya.
“Wadau kwa mlivyo pambana kwa muda wote huo ambapo mkoa ulitangazwa kuwa unaongoza kwa maambukizi najua bila shaka maambukizi yatakuwa yameshuka lakini takwimu za kitaifa hazijatoka inaumiza sana naomba wahusika watoe takwimu mpya naamini Tutakuwa tumepunguza maambukizi,” alisema Saitabahu
Alisema kuwa Wadau mkoa wa Njombe wamekuwa wakipambana kila kukicha jinsi ya kushusha maambukizi ya Ukimwi na kuna uhakika wa kushika kwa maambukizi na kuwa lengo ni kufikia ziro tatu ambapo maambukuzi mapya ziro, Unyanyapaa Ziro na vifo vitokanavyo na Ukimwi Ziro.
“Najua mtakuwa mnajua kutokana tathimini zenu wenyewe mnako fanya kazi watu walio Pima na wanao gundulika na maambukizi najua mtakuwa na majibu na mnajua yameshuka licha ya kuwa haturuhusiwi kutangaza kuwa tumeshuka kwa maambukizi lakini mpaka utafiti ufanywe na Tacaids ndio takwimu zitolewa,” aliongeza Saitabahu.
Aidha mratibu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Tacaids, mkoa wa Njombe Abubakari Magege, alisema kuwa mwaka ujao kuna mpango wa kuanza kufanya utafiti wa maambukizi ya Ukimwi na Malaria nchi nzima na kuwa takwimu mpya ndipo zitatolewa.
Alisema kuwa wamekuwa wakipambana kila kukicha kutoa elimu katika maeneo mbalimbali hasa maeneo hatarishi na kuwa utafiti huo utatoa sura halisi ya maambukizi ya Ukimwi kwa mkoa wa Njombe.