Lee Kuan Yew afariki dunia


Waombolezaji wakiweka mashada ya maua mbele ya hospitali aliyofia baba Lee Kuan Yew.
Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia.Lee amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa mapafu.
Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha kimataifa.
David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini humo, ametuma salamu zake za rambi rambi.Kifo cha Lee ni mwisho wa zama zake.mwisho wa mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani katikati ya miaka ya sitini .
Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata leo na unaweza kuvuka mipaka sio kwa singapore tu bali hata kwa watu wa Asia ya kusini Mashariki.