WAFANYIKAZI KUSALIA MAJUMBANI LIBERIA.


Rais wa Liberia Johnson Sirleaf
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf amewaagiza wafanyikazi wa serikali wasio na umuhimu mkubwa kusalia majumbani mwao kama mpango wa serikali wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Wafanyikazi hao walitakiwa kueneza kampeni za kuwahamasisha watu kuhusu ugonjwa huo katika makaazi yao.
Maafisa wa afya kutoka nchini Marekani wakati huohuo wamesema kuwa wana hakika kwamba kisa cha kwanza cha ugonjwa huo nchini humo kinatokana na mtu mmoja aliyerudishwa kutoka Liberia na kwamba kitadhibitiwa.
Liberia ndio taifa liloathirika vibaya na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umewaua zaidi ya watu elfu tatu katika eneo la Afrika magharibi