kundi la Al Nusra Front latangaza vita

Wapiganaji wa Jihad kutoka kundi la Al Nusra front
Kundi lililo na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda nchini Syria Al- Nusra Front limepinga mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na muungano unaoongozwa na Marekani kama vita dhidi ya Uislamu na kusema kuwa nchi za magharibi na zile za kiarabu zinazohusika zitalengwa na makundi ya Jihad kote duniani.
Matamshi hayo yanatolewa baada ya Marekani kusema kuwa ushirikiano na washirika wake wa kiarabu umefanya mashambulizi zaidi dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria na Iraq.
Wizara ya ulinzi nchini Marekani ilisema kuwa ndege za kijeshi zilishambulia mji wa Raqqa nchini Syria ambao ni ngome ya wanamgambo pamoja na maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Islamic state karibu na mji wa Kikurdi wa Kobane karibu na mpaka na Uturuki.