Akuwa pembezoni mwa Kanisa akiwa ameuwawa Njombe







MKAZI wa Melinze kata ya Mjimwema Mkoani Njombe, Evaristo Mgeni amekutwa pembezoni mwa kanisa akiwa amefariki dunia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Melinze, Mkoani Njombe, eneo la tukio wamesema kuwa Mgeni walimkuta pembezoni mwa uzio wa kanisa la Lutheran akiwa amekufa.

Afisa mtendaji wa Kata ya Mjimwema, Geazi Kongwa alisema kuwa alipokea simu kutoka kwa afisa mtendaji wa mtaa wa Melinze akimtaka kufika katika eneo la Tukio majira ya saa 2:30 asubuhi.

Alisema kuwa alipo fika eneo la tukio aliukuta mwili wa marehemu ukiwa umezungukwa na watu ambao walikuwa ni wapita njia na ndipo alipo piga simu polisi ili kuja kuuchukua mwili huo.

Alisema "Nilipofika hapa niliona hakuna dalili ya kuja Polisi nikapiga simu polisi Ndipo jeshi hili limefika katika eneo la Tukiona kuuchukua mwili wa marehemu ambao haujakutwa na majeraha ya aina yoyote,"

Aidha afisa huyo alisema kuwa marehemu inasadikika kuwa alikufa majira ya usiku sana marehemu alikutwa na simu ambayo ilikuwa ikiita mfukono mwake.


Baada ya jeshi la Polisi kufanya upekuzi katika mwili wa marehemu alikuwa akiwa na simu moja na katika pochi yake alikuwa na shilingi elfu moja.

Nae  mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina moja la, Mgeni mfanyabiashara Melinze, alisema kuwa kijana huyo anamfahamu na amekuwa akipita mara kwa mara katika maeneo hayo ya kanisa mara nyingi amekuwa akionekana wakati wa kwenda tu na wakati wa kurudi ni marachache sana.

Alisema kuwa marehemu alikuwa akiishi na shangazi yake maeneo ya Melinze na mara nyingi alikuwa akitoka na kuelekea Chaugingi.

Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, wakiwepo na ndugu wa marehemu kuelekea Hopitali ya mkoa wa Njombe Kibena kwaajili ya Uchunguzi zaidi.

habari na Mwandeshi wetu Elimtaa