Takriban wakwea milima 30 huenda wameaga dunia nchini Japan
kufuatia kulipuka kwa mlima wa Volcano siku ya Jumamosi na kusababisha
kukwama kwa mamia ya raia hao karibu na kilele cha mlima huo
Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha mlima Ontake.
Wakwea milima katika mlima Ontake
Waokoaji hao wamefanikiwa
kufika kwenye kilele cha mlima huo ambapo ndege ya kijeshi aina ya
helikopta ilitumiwa kuwaokoa karibu watu 40 waliokuwa wamejeruhiwa
Zaidi
ya wakwea milima 200 walifanikiwa kuteremka kutoka kwa mlima huo wenye
urefu wa mita 3000 wakati mlima huo ulipoanza kutupa mawe na majivu bila
ya kutoa onyo lolote.
Baadhi yao walisema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.