Showing posts with label JAPAN. Show all posts
Showing posts with label JAPAN. Show all posts
Picha za bomu la nyuklia Nagasaki Japan

Picha za bomu la nyuklia Nagasaki Japan


Bomu ya kiatomiki ilipolipuka mjini Nagasaki
Huku ulimwengu ukiadhimisha miaka 70 tangu ndege za kijeshi za Marekani ilipodondosha bomu la kinyuklia juu ya Nagasaki tazama picha za janga hilo.
Majengo yote na viwanda viliharibiwa kabisa
Ibada maalumu za ukumbusho zinaendelea kufanywa katika mji wa Nagasaki, nchini Japan, kuadhimisha miaka 70 tangu kulipuliwa kwa bomu ya atomiki jijini humo.
Zaidi ya watu elfu 70,000 waliangamia
Wahasiriwa wa bomu hilo waliungua mwili wao mzima
Tarehe 9 Agosti mwaka wa 1945, ndege ya Marekani ikiwa imejihami kwa silaha zenye nguvu za kitonaradi ilidondosha bomu la pili kuwahi kutupwa katika uwanja wa kivita katika mji wa , Nagasaki ambao ulikuwa ndio kitovu cha uzalishaji wa viwanda nchini Japan.
Siku 6 tu baadaye Japan ilitangaza kuwa imejisalimisha katika vita hivyo vya dunia.
Siku 6 tu baadaye Japan ilitangaza kuwa imejisalimisha katika vita hivyo vya dunia.
Watu 74,000 waliangamia
Takwimu zinasema kuwa takriban watu 74,000 waliangamia.
Watu wengi zaidi walikufa kutokana na athari ya miale ya nyuklia
Hii ilikuwa ni idadi kubwa zaidi ya watu hususan ikitokea siku tatu tu
Asilimia 70 ya watu hawakuwa na makao
baada ya bomu la kwanza la kinyuklia kuua zaidi ya watu 140,000 mjini Hiroshima.
Bomu hiyo iliyotikisa na kuangamiza kabisa mji wa Nagasaki
Bomu hiyo iliyotikisa na kuangamiza kabisa mji wa Nagasaki ilijulikana kwa jina la utani kama ''Fat Man''.
Wahasiriwa wa mkasa huo hawataki Japan ijiuhusishe na vita tena
Ndege iliyotumika kutupa bomu hilo ilijulikana kama Bockscar, ilipaa kutoka kisiwa cha Mariana.
Kanisa kubwa zaidi wakati huo liliharibiwa kabisa
Rubani wake alikuwa Meja jenerali Charles Sweeney.
Zaidi ya watu 200,000 waliuawa
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000 waliuawa katika milipuko hiyo miwili,
Wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi
Wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi.
Viongozi wanamkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa kubadili sera na katiba ilikuiruhusu nchi hiyo kushiriki kwa vita
Katika ibada ya ukumbusho iliyoandaliwa leo mjini Nagasaki,
Ndege iliyotumika kutupa bomu hilo ilijulikana kama Bockscar
wahasiriwa walimzomea waziri mkuu wa bwana Shinzo Abe kwa kutaka kubadilisha katiba ya taifa hilo ilikuwaruhusu wanajeshi wa Japan kuhusika na mapigano.
Mnara wa amani umejengwa katika eneo hilo
Meya wa mji wa Nagasaki naye alivutia waya huohuo akimkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa jitihada za kubadilisha katiba ya nchi.

MATEKA MWINGINE WA KIJAPANI AUAWA KWA KUCHINJWA SHINGO NA KUNDI LA KIISLAM LA ISI BAADA YA JAPAN KUKATAA KUTOA HELA


Taarifa za hivi punde zinabainisha kuwa mwandishi wa habari raia wa Japan aliyekuwa akishikiliwa na kundi linalojiita Islamic state of Iraq and the levant ameuawa kwa .....
kuchinjwa Shingo na kundi hilo..
Awali ISIL ilihitaji dola million Mia mbili kama kikombozi (ransom) ili kumwachia huru madai yaliyopingwa na Japana
Kenji goto anakuwa mjapani wa pili kuuawa katika kipindi cha mwezi mmoja na kundi hilo
Jivu la Volkano lawaua watu 30 Japan

Jivu la Volkano lawaua watu 30 Japan

 
Mlima Ontake
Takriban wakwea milima 30 huenda wameaga dunia nchini Japan kufuatia kulipuka kwa mlima wa Volcano siku ya Jumamosi na kusababisha kukwama kwa mamia ya raia hao karibu na kilele cha mlima huo
Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha mlima Ontake.

Wakwea milima katika mlima Ontake
Waokoaji hao wamefanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima huo ambapo ndege ya kijeshi aina ya helikopta ilitumiwa kuwaokoa karibu watu 40 waliokuwa wamejeruhiwa
Zaidi ya wakwea milima 200 walifanikiwa kuteremka kutoka kwa mlima huo wenye urefu wa mita 3000 wakati mlima huo ulipoanza kutupa mawe na majivu bila ya kutoa onyo lolote.
Baadhi yao walisema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.
 
 

Kategori

Kategori