SERIKALI kote nchini imeamua kufanya zoezi la kuwahakiki
wastaafu wote walioitumikia serikali waki hii ili ili kupata takwimuhalisi ya
watu waliopo baada ya wengine kufariki dunia.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa hazina ndogo mkoani Mbeya
Stanford Siwale jana jijini Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake kuhusiana na kazi ya uhakiki wa wastaafu hao inayo endelea mkoani
Mbeya.
Siwale alisema kuwa kutokana na ratiba iliyo tolewa na Wizara
ya Fedha jijini Dar es salaam zoezi hilo lilianza Machi 3 na kumalkizaka Machi
14 mwaka huu.
Alisema kuwa idadi ya
siku za usahili kwa halmashauri itategemeana na wingi wastaafu waliopo katika
halmashauri husika na kuwa katika halmashauri ya Mbarali uhakiki ulifanyika kwa
siku moja ambayo ina wastaafu 11 pekee kuwa zoezi litafanyka kwa siku moja tu.
“Mfano katika halmashauri ya wilaya ya Chunya kuna wastaafu
wanaoishi katika maeneo ya vijiji kama vile Kambikatoto, Namkukwe na
Bitimanyanga, ambavyo vipo yapata zaidi
ya kilomita 200 kutoka makao makuu ya wilaya ya chunya,” alisema Siwale
Siwale aliongeza kuwa hatakama utaratibu huo ungepangwa
mapema lakini bado zoezi hilo linge chelewa, kwa sababu wengi wa wastaafu sio
waajiliwa hivyo kuwapata inakuwa vigumu.
Kwa upande wao wastaafu walisema kuwa nia ya serikali ya
kufanya uhakiki kwa watu wanao ishi sio mbaya, kwa sababu inataka isiwe inatoa
mafungu kwa watu ambao ni wafu.
Kauli hiyo ilitolewa na mzee Maclean Mwangomale ambaye ni
mkazi wa Forest Jijini Mbeya, na kuongeza kuwa mpango wa kuwaita wazee kwenye
uhakiki haukuandaliwa vizuri kwani umejaa usumbufu.
Mzee Alford Kasule Mkazi wa Nzovwe, alisema kuwa zoezi hilo
sio baya ila utaratibu unaotumika si mzuri, kwa sababu ofisi inayo toa huduma
ambayo ni ya jiji ni moja hali inayo sababisha washinde kwenye foleni kutwa
nzima.
Naye Oswald Malofwa wa Nzovwe ameiomba serikali inapo andaa
program ya namna hii iwe inawaandalia na alawansi ya posho, kutokana na
matatizo wanayo yapata wakati Sajenti mstaafu Duncan Mponda naye amelalamikia
kiwango wanachopewa kuwa ni kidogo
kutokana na ugumu wa maisha.
Mstaafu mwanamke Nabwike Mwasumbwe m kazi wa mkazi wa
Mwanjelwa ameiomba serikali itafakali sana juu ya utendaji wake kwa wastaafu,
ambao wamedai waliitumikia serikali yao kwa utiifu mkubwa lakini leo hii
serikali haiwathamini.
Wastaafu wengine wamesema kuwa pesa wanayolipwa kwa sasa na
serikali ya shilingi 150,000/= kama mafao yaani shilingi 50,000/= kwa mwezi,
haitoshi kabi sa ukizingatia ugumu wa maisha.