MATUKIO YAPUNGUA MBEYA KWA ASILIMIA KAZAA

MATUKIO ya ajali za barabarani yamepungua kwa asilimia 24 kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Januari mpaka mwishoni mwa Februari.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema kuwa matukio ya ajali za barabarani yamepungua kwa asilimia 24 kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Akitoa takwimu hizo Msangi alisema kuwa mwezi Januari kulikuwa na matukio 38 na kupungua hadi kufikia matukio 29 Februari mwaka huu.

Alisema kuwa katika ajali hizo zilizo sababisha vifo ni ajali 27 kwa mwezi Januari na kuwa yamepungua mpaka 15 Februari na hivyo kuw akunapungufu ya matukio 12 ambayo alisema kuwa ni sawa na asilimia 44.

Msangi alisema kuwa kwa kipindi hicho kuna jumla ya upungufu wa vifo kwa asilimia 40 ambapo alisema watu 30 walikufa kwa kipindi cha Januari na Februari watu 18 ambapo kuna upungufu wa wa watu 12.

Akifafanua zaidi kuhusiana na upungufu wa matukio mbalimbali ya kiharifu na ajali mkoani Mbeya alisema jumla ya makosa 3,788 yalitokea mwezi februali ambayo yalikuwa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na yalitozwa faini na tozo la shilingi mil. 100.9.

Alisema kuwa kufuatia kiasi hicho kimefungua kutoka shilingi mil. 131.3 kwa wezi Januari ambayo ilikusanywa kutoka makosa 4,378 sawa na asilimia 23.

Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi ili kupunguza matukio yanayo tokea katika mkoa wa Mbeya.