CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Mbeya kimetoa kauli kuhusiana na
Shitaka la Zitto kuipeleka Chadema mahamanani na kusema kuwa sio mwenzao.
Akizungumza na Nipashe jijini Mbeya mwenyekiti wa Chadema
Vijana, Joseph Kasambala alisema kuwa kitendo cha mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto
Kabwe kukipeleka chama hicho mahamani ni sawa na kufanya usaliti.
Alisema ni bora Zitto akafukuzwa uanachama na kwenda
mahakamani alifanya uamuzi huo kwa haraka na alipaswa kukata rufaa kufuatia
maamuzi ya kamati kuu kabla ya kwenda mahakamani.
Kasambala alisema kuwa kamati kuu ya Chama hicho ilimuita
kujieleza na hakufanya hivyo na kukimbilia mahakamani kitu ambacho ni kinyume
cha katiba ya chama hicho.
“Bora chama uongozi ukafanya maandalizi ya kuchukua nchi kwa mwaka 2015 na katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuliko kupoteza mda katika kufanya kazi ya kuzungumzia masuala na mtu asiye na manufaa kwa chama,” alisema Kasambala.
Alisema kuwa Katiba ya chama inaweza kumfukuza mwanachama
yeyote Yule kama ataenda kinyume na chama hicho kwa kuto jail umaarufu wa
mwanachama huyo.
Kasambala alisema Zitto kuwa mbunge asiyehuzulia katika vikao
vya chama hicho ni bora akawa hivyo kuliko kuwa na mtu ambaye anafanya mambo ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa ndani ya Chadema.
“Ni zambi kufanya mambo ya CCM ukuwa Chadema na bora mtu kutoka CCM kwenda Chadema,” alisema Kasambara.