Lowassa Kuzindua Kampeni ya ‘ TOROKA UJE ’ Leo


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kushirikiana na UKAWA leo wanatarajia kuzindua kampeni nyingine iliyopewa jina la ‘Toroka Uje’ katika viwanja vya Tanganyika Pekazi Kawe jijini Dar es salaam.
 
Habari za ndani zinaeleza kuwa kampeni hiyo inatarajiwa kuwa ya aina yake katika dakika za mwisho kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25, 2015.
 
Uzinduzi huo ulipangwa kufanyika jana lakini  ukaahirishwa kuruhusu watanzania wengi kushuhudia  tukio hilo.
Mpekuzi blog