JESHI
la Polisi Mkoani Mbeya limekamata Jumla ya Lita nane kutoka katika
maeneo mbalimbali Mkoani Hapa Ikiwa ni pamoja na mtu mmoja kukamatw ana
lita tatu jijini Mbeya.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Mbeya Kamanda wa Pilisi Mkoa wa Mbeya
Ahmed Msangi (Pichani). alisema kuwa Matukia hayo ya watu kukamatwa na gongo
walikutwa kutoka katika wilayambalimbali mkoani Mbeya wakiwa na ujamzo
mbalimbali.
Alisema
kuwa katika tukio la Kwanza jeshi la Polisi lilimkamata Tukulamba
Aston, mtuhumiwa alikamatwa jijini Mbeya na lita tatu za Pombe ya Moshi
maarufu Gogo.
Alisema mtuhumiwa huyo mkazi wa Mafiati jijini Mbeya ni mtumiaji na muuzaji wa Pombe hiyo ambayo inapigw avita na serikali.
Alisema
kwua katika tukio la pili Jechi la Polisi lilikamata lita mbili katika
kijiji cha Katumba wilayani Rungwe walimkamata Vick Emanuel (20) akiwa
na pombe hiyo.
Alisema kuwa mtuhumiwa ni mtumiaji na muuzaji wa Pombe hiyo katika maeneo ya Katumba Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Hapa.
Msangi
alisema kuwa Pia polisi walipo kuwa dolia katika maeneo ya Iyunga
jijini Mbeya walimkamata Suma Mwampiki mtumiaji na muuzaji walimkuta na
Lita moja na Nusu na taratibu za kumfikisha katika vyombo vya sheria
zainafanywa.
Aliongeza
kuwa jeshi la polisi liliingia katika maeneo ya vilabu maeneo ya Uyole
lilikamata lita moja na nusu ambazo zilikutwa na Joseph Mwakisa ambaye
ni muuzaji na mtutumiaji na muuzaji kilabuni hapo.