DEREVA NA ABILIA WAFA AJALINI

DEREVA wa Pikikiki maafuru kama Bodaboda amefariki dunia papo hapo akiwa na abiria wake baada ya pikipiki hiyo kugonga kwa nyuma Lori kwa nyuma  katika maeneo ya Sae jijini Mbeya.

Ajali hiyo iliutokea juzi katika maeneo ya Sae jijini Mbeya barabara ya Mbeya /Njombe Bodaboda iligonga gali kwa nyuma gari aina ya Scania yenye namba za usajili T.684 BVY.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi (Pichani) alisema kuwa tukio hilo lilihusisha Pikipiki na Loli.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya aliwataja marehemu hao kuwa ni Gabiliel Ngalele (24)  Mkazi wa Uyole jijini Mbeya na abilia wake hakufahamika jina.

Akisimulia tukio hilo alisema kuwa Pikipiki iliyokuwa na abaria iligonga Loli kwa nyumba.

Alisema kuwa tikio lilitokea kutokana na mwendokasi wa Pikipiki ambayo ilikuwa ikitokea Uyole kuingia katikati ya jiji la Mbeya.

Alisema kuwa Lori hilo dereva wake hakupatika na na hajafahamika jina lake ambapo alitokomea kusiko julikana.

Kamanda Polisi Mkoa wa Mbeya Msangi alisema kuwa madereva wawe makini watumiapo vyombo vya moto barabarani.