Kauli hiyo aliitoa jana ofisini kwake baada ya kupatiwa taarifa kuwa
kumekuwepo na tabia ya viongozi hao kutumia mali ya serikali kwa ajili
ya kujinufaisha wao bila kujali masilahi wa wananchi.
Alisema kuwa kumekuwepo na tabia ambayo watendaji wa kata na vijiji
kuhamisha madeni ya ushuru kutoka katika kitabu kimoja hadi kingine
jambo ambalo linaisababishia wilaya hiyo kukosa mapato ya ndani kwa
wingi.
Mwala alisema kuwa watendaji hao wamekuwa na kauli za kejeli kuwa
hauwezi hufanya kazi bila ya kuwa na madeni na kujigamba kwa kuwa na
vitabu viwili ambapo ni kinyume na sheria zilizo wekwa na ukiukwaji wa
maadili ya kazi zao.
“Kuanzia sasa maafisa watendaji wa kijiji na kata watachukuliwa hatua
za kisheria pindi watakapo kuwa wamekutwa na tuhuma za kutumia mali ya
serikali bila ya kibali maalumu na kufukuzwa kazi zao ilikuweza
kukusanya mapato mengi kwa wilaya hii” alisema Mwala.
Alisema kuwa kuanzia sasa kutakuwepo na opalesheni ya kuwakagua
maafisa watendaji wa kata na wavijiji ilikuweza kubaini wanao tumia
mali hizo za serikali kinyume na walivyo kuwa wakiapa kiapo cha
kuitumikia serikali yao.
“Vinginevyo tutawafukuza wote watendaji wa kata na vijiji ambao
wanafanya kazi ya kuujumu mali ya serikali na tukabakia na makaimu
watendaji ambao watafanya kazi kwa uhakia na haita kuwa ni jambo la
ajabu kwetu maana kuna wilaya hapa nchini iliwahi kufukuza watu wa
namna kama hiyo” alisema Mwala
Aliongeza kuwa halmashauri hiyo imekuwa ikikusanya mapato kidogo kwa
sababu watendaji wamefanya miradi ya serikali kuwa mali yao na ushuru
umekuwa ukikusanywa kwa wingi kiasi kinacho lejeshwa halmashauri ni
kidogo.