TREKTA LAGONGANA NA PIKIPIKI ABILIA AFA
WATU wanne wamefariki dunia
katika ajali tatu tofauti zikiwemo mbili za pikipiki jijini Mbeya katika wilaya
za Rungwe na Mbozo Mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa
habari Mkoani Mbeya Kamanda wa Polisi Ahmed Msangi alisema kuwa katika ajali ya
kwanza iliyo tokea wilayani maeneo ya Ichenjeza wilayani Mbozi watu wawili dereva
bodaboda, Haruna Jacob na abilia wake Kelvin Jacob wafamilia moja waligongana
na gari mali ya Ilasi Sekondari aina ya Coaster.
Alisema gari hiyo yenye namba
za usajili T 784 AVB ilikuwa ikiendeshwa na Godfrey Mwalingo mkazi wa
UIchenjeza iligonga na Pikipiki yenye namba za usajili T 268 CTR na kusababisha
vifo vya watu hao miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya
Mbozi
Msangi alisema kuwa katika
ajali ya pili gari aina ya Mitsubishi Canter iliacha njia na kupinduka kisha
kusababisha kifo cha Anangisye Stewat (27) mkazi wa Ikuti jijini Mbeya ambaye
alikuwa Tingo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Mbeya.
Alisema kuwa dereva katika
ajali hiyo hajafahamika na ajali hiyo imetokea majira ya saa 1: 30 usiku wa
jana, katika maeneo ya namba One wilayani Rungwe mkoani hapa.
Msangi aliongeza kuwa katika
ajali ya tatu Pikipiki iligongana na Treka maeneo ya Kayuti wilayani Rungwe na
kusababisha kifo cha babilia wa Pikipiki hiyo Alfa Mndendemi (24) mkazi wa
Mkoani Njombe wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Makandana wilayani humo.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi huku chanzo cha ajali hiyo ikionyesha kuwa ni wendo kasi wa trekta ambalo liliigonga pikipiki hiyo, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya makandana.