RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza bohari ya
chakula nchini kufungua maghala yake ili chakuka likichomo kipelekwe kwa watu
walioathiriwa na mafuriko katika tarafa ya Magole mkoani Morogoro.
Pia aliamuagiza Waziri anayeshughuliki
maafa, Willium Lukuvi, kuhakikisha waathirika wa mafuriko wanasaidiwa haraka
ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba.
Akizungumza na waathirika wa mafuriko katika
skuli ya sekondari Magole baada ya kukagua athari za mafuriko, Rais Kikwete
alisema mbali na waathirika kupata baadhi ya misaada, serikali itafungua
maghala yake na kuwasambazia chakula.
“Hili la chakula na makazi ondoeni
shaka,kwanza tunakwenda kufungua ghala letu la taifa na kama kutakuwa na
upungufu wa aina yoyote ya chakula serikali itanunua kujazia, kuhusu makazi
naliagiza Jeshi la Wanachi kuanza kazi hii mapema maana tukiwapa kazi hii halmashauri watu wataishia
kujenga nyumba zao tu,” alisema.
Akionyesha imani ya utendaji bora na
nidhamu katika matumizi ya fedha za umma,
alisema kwa kuanzia zitajengwa zaidi ya nyumba 200 za mabati juu na
chini na kuwagawia.
Akionyesha kutofurahishwa kwa mpango wa
dharula wa kuwaweka wanaume mbali na wanawame pasipokujali nasaba zao,
aliwataka Wakuu wa mikoa iliyokumbwa na mafuriko,Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi
wao kufanya tathimini ya kina juu ya waathirika na malizao ili serikali iweze
kuwasaidia.
Aidha ameviagiza viwanda vya magodoro nchini kupeleka magodoro kwa waathirika hao ili waepukane na kulala chini kwenye unyevunyevu.
Na Farida Msengwa,Magole, ZanziNews