Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akifunua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa Soko la Kuuzia Samaki la liliopo Unguja Ukuu Kaepwani
litakalotoa huduma kwa Vijiji vya Uzi, N’gambwa na Unguja Ukuu yenyewe.
Balozi Seif akiwa pamoja na Viongozi wa
Mkoa wa Kusini Unguja, Jimbo la Koani na Wananachi wa Unguja Ukuu
Kaepwani akiangalia baadhi ya sehemu ya jengo la Soko ya Kuuzia samaki
liliopo pembezoni mwa ufukwe wa Kijiji cha Unguja Ukuu Kaepwani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Unguja Ukuu Kae Pwani
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo jipya la kuuzia samaki
katika Kijiji hicho.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Malozi Seif Ali Iddi alisema katika kuunga
mkono nguvu za Wananchi za kujiletea maendeleo katika maeneo yao mbali
mbali Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kusaidia miradi ya
kiuchumi na kiustawi wa Jamii ili kuona juhudi za Wananchi hao zinafikia
kwenye maendeleo yaliyokusudiwa.
Balozi
Seif alieleza hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Unguja Ukuu
Kaepwani mara baada ya kuweja Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Soko ya
Kuuzia Samaki liliopo pembezoni mwa Bahari ya Kijiji hicho ambalo
linajengwa kwa nguvu za Viongozi na Wananchi wenyewe.
Balozi Seif Ali Iddi lisema Serikali itajitahidi kuona jengo hilo
linamalizika kwa wakati na akawataka wananchi hao wamalizie ujenzi wa
vibaraza vya ndani ya jengo hilo ambapo yeye binafsi aliahidi kuchangia
shilingi Laki 500,000/- kutekelezwa kazi hiyo ili kuipakasi Serikali
Kuu imalizie masuala yaliyobakia.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza wananchi hao kwamba Serikali pia
itajitahidi kuwapatia boti maalum kwa ajili ya uokozi wa wavuvi pale
inapotokea ajali wakati wakiwa katika shughuli zao za uvuvi.
Aliwapongeza
Wananchi hao kwa uwamuzi wao wa kujenga jengo la kudumu la kuuzia
samaki na kusisitiza kwamba maeneo ya uvuvi ni lazima wakati wote yawe
katika mazingira bora.
Akisoma
risala ya Wananchi wa Jimbo la Koani Mwalimu Makame Haji Steni alisema
ujenzi wa soko hilo umekuja kufuatia tatizo kubwa la mauzo ya samaki
lililokuwa likiwakumba wavuvi wa maeneo hayo.
Mwalimu
Makame alisema wavuvi hao walikuwa wakilazimika kuuza samaki wao masoko
na Mjini kitendo ambacho kilikuwa kikiwakosesha mapato makubwa na
kujikuta wakipata hasara.
Ujenzi
wa soko hilo ulioanza mwaka 2013 umefikia gharama ya shilingi Milioni
11,000,000/- zilizotokana na mchango wa Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la
Koani kwa ushirikiano wa nguvu za Wananchi wenyewe.
Soko hilo la kisasa litakapokamilika linatarajiwa kuhudumia wavuvi wa Vijiji vya N’gambwa, Uzi na Unguja Ukuu yenyewe.
Na ZanziNews